Na Fauzia Mussa , Maelezo

Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Ali khamis Juma amesema watoto wenye ulemavu ni sehemu ya jamii na wanahitaji kupata fursa ya kuonesha vipaji vyao.

Akizungumza katika Bonanza la Michezo kwa watu wenye ulemavu huko viwanja vya Mao Zedon'g Katibu huyo amesema watoto hao wanahaki ya kushiriki katika michezo kama watoto wengine hivyo mashirikiano ya pamoja yanahitajika ili kuwasaidia kuipata haki hiyo.

Aidha aliwataka Watendaji wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu kushirikiana na Wizara ya Elimu na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ili kuhakikisha watoto hao wanapata fursa za kushiriki katika mabonanza na kuonesha vipaji vyao.

Katibu Ali aliwapongeza wazazi walioongazana na watoto hao kwa kuwawezesha kushiriki michezo kwani bila ya mashirikiano yao wasingeweza kufika viwanjani hapo.

“Mtoto mwenye ulemavu hawezi kushiriki michezo kama wazazi wake hawapo tayari, nawashukuru wazazi waliowaleta watoto wao hapa na nashauri wazazi waliokaa majumbani kuwatoa watoto wao kwani wanahaki kama watoto wengine”Alisema Katibu huyo

Hata hivyo aliwataka watu wenye ulemavu kushirikiana kwa pamoja ili kudai na kutetea haki zao kwa misingi ya amani.

“Nyinyi ni mashujaa msikubali kuonewa wala kudhulumiwa shikamaneni mdai kila haki yenu” alisisitiza Katibu Ali

Vile vile aliyataka Mabaraza ya Watu wenye Ulemavu ya Wilaya kuanzisha vilabu vya michezo katika Wilaya zao ili kutoa fursa kwa watu wenye ulemavu kushiriki michezo kwani michezo hutoa fursa za ajira.

Akitoa maelezo mafupi Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la watu wenye ulemavu Ussy Dede alisema bonaza hilo ni miongoni mwa shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu ambayo huadimishwa kila ifikapo Disemba 3 Dunia kote.

Nao washiriki wa Bonanza hilo waliiomba jamii kuendelea kujifunza lugha za alama ili kuwasaidia watu wenye ulemavu wa uziwi kwani wamekuwa watu wa mwisho kupata taarifa.

Katika Bonanza hilo michezo mbalimbali ilichezwa na watu wenye ulemavu ikiwemo mbio fupi za Mita Mia,mbio za magunia,mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu wa viungo,kuvuta kamba,nage, na golbal kwa watu wenye ulemavu wasioona.


K

atibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda  Ali khamis Juma akizungumza katika bonanza la michezo kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya walemavu ambayo hufanyika Kila ifikapo Disemba 3 Duniani kote
 

 Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la watu Wenye Ulemavu Zanzibar Mhandisi Ussy Khamis Dede akizunguma machache na kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanada kuzindua Bonaza la Michezo kwa watu wenye Ulemavu huko viwanja vya Mao Zedong ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu ambayo hufanyika Kila ifikapo Disemba 3 Duniani kote.
 

Watu wenye Ulemavu wa akili wanaume SOZ wakiwa katika mashindano ya mbio za Mita mia katika bonanza la michezo kwa watu wenye ulemavu  ambapo Abdul Khatib aliibuka mshindi wa kwanza , ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu ambayo hufanyika Kila ifikapo Disemba 3 Duniani kote.

Timu ya mpira wa miguu  ya Watu wenye ulemavu wa viungo Wilaya ya Mjini wakichuana na Magharibi A ambapo Magharibi A waliibuka na ushindi wa bao 2-1 ,katika bonanza la michezo kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu ambayo hufanyika Kila ifikapo Disemba 3 Duniani kote.

 

PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...