DIWANI wa Kata ya Ukonga Ramadhani Bendera amewataka wazazi kushirikiana na serikali katika kuhimarisha malezi na maadili ya watoto wao ili kuweza kuzuia tabia zisizofaha zinazotokana na makundi rika.

Bendera ameyasema hayo katika mahafali ya 17 ya wanafunzi wa kidato cha nne ya Shule Huria ya Ukonga Skillfull ambapo amesema Serikali inajitahidi kutengeneza mazingira mazuri na bora kwa watoto ili kuondoa au kuzimaliza kabisa tabia zitokanazo na makundi rika.

Amesema ili kuunga mkono jitihada hizo za serikali za kuziondoa tabia hizo ni vema wazazi wakatambua kuwa wanapaswa kuziondoa kuanzia majumbani mwao.

''Kuna tabia nyingi chafu zinazofanywa na watoto hali hii imetufanya sisi kama Kata kuja na wazo la kutegeneza kamati ambayo inashughulika na changamoto za watoto katika shule zote zilizopo katika kata yetu ambapo kamati hiyo itakuwa inasimamiwa chini ya mtendaji kata itakayoanza kupita mashuleni,''alisema na kuongeza

''Sasa sisi tukiwa tunahudumia mashuleni ,wazazi tunaomba muhakikishe mnahudumia majumbani mwenu hapo ndipo itasaidia sisi kwa pamoja kushirikiana katika kumlea mtoto mzuri.

''Leo hii msione mie nimefika hapa mkajua nimekurupuka tu ,nimelelewa vizuri na jamii ya wanaukonga ambapo ndipo ninapoishi na nilipozaliwa,hivyo mtoto alelewi na mzazi pekee yake bali na jamii inayomzunguka ,''amesema.

Kwa Upande wake Muasisi wa Shule Huria ya Ukonga Skillfull, Diodorus Tabora amesema mahafali hayo ni ya 17 tangu shule hiyo kuanzishwa kwake ambapo takribani wanafunzi 200 wanatarajia kufanya mitihani ya taifa ya kidato cha nne .


Amesema shule yao imejikita katika nguzo tatu ikiwemo kuhakikisha wanafunzi wanakuw na nidhamu, wanamjua Mungu na kuwa na hofu ya Mungu na ufundishaji wenye weledi.


''Wazazi na walezi niwaombe kuacha kuwakatia tamaa watoto hawa ambao wamefeli kidato cha nne na kuja kurudia mtihani, mnapaswa kuwasaidia katika kuwapa ushauri ambao utawafanya warudie mitihani yao na kuweza kupata alama za juu kabisa,''amesema

Amesema miaka ya sasa wazazi na walezi wengi wamekuwa wakiwadekeza watoto wao hali inayowafanya kutokuwa wakakamavu kama miaka ya nyuma.

Aidha amesema suala la maadili sasa hivi limekuwa janga kubwa kimataifa hivyo ni lazima wapigane nalo ili kuhakikisha wanawalinda watoto wao katika maadili yaliyomema na mazuri ambayo yatakuja kuwaletea manufaa miaka ya baadae wanapokuwa wakubwa.

''Wazazi muache kuwadekeza vijana wenu,mkae nao na kuhakikisha mnawalea katika maadili yaliyomema muache kuwadekeza kwani vijana wa sasa wanaishi maisha feki ,mzazi au mlezi usimshindwe mtoto wako unapaswa kumwambia ukweli,''alisema na kuongeza

''Tujitahidi kuwalea watoto wetu katika misingi mizuri,kwani hata hizi tabia zinazotoka huko nchi nyingine na kuingia nchini ndo hizi zinazowaharibu watoto wetu,''amesisitiza.

Hata hivyo amesema wazazi wengi wameshindwa kufanya jukumu la malezi kwa kutokuwa karibu na watoto wao, wengi wakikimbizana na jukumu la kutafuta fedha jambo ambalo wakati fulani linawapa wakati mgumu walimu kuwa karibu na watoto kama walivyo wazazi.

"Ni muhimu wazazi kutumia muda mwingi kuwa karibu na watoto wao, mnapowapeleka shuleni zingatie kuwafatilia kila hatua yanayopitia hiyo itasaidia hata katika ufahulu wao, tumieni muda huo kuwaonyedha pia uhalisia wa maisha jinsi ulivyo, wasijaribu kuishi maisha ya mitandaoni yaani fake life ambayo kwa sasa ndiyo yanawatesa vijana wengi nchini," alisema



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...