Na John Walter -Manyara
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amempitisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Suleimani Jafo kuona Magugu Maji yalivyovamia ziwa Babati na kupoteza mvuto wake.
Ziwa hilo linalotegemewa na wakazi wa Mjini Babati Kwa ajili ya kupata kitoweo Cha Samaki limezingirwa na Magugu hayo jambo linalopunguza ukubwa wa ziwa.
Sendiga alimtembeza Waziri huyo naye ajionee kasi ya uvamizi huo na jitihada zinazoendelea za kuyaondoa magugu maji hayo kwa kutumia mikono ambazo huenda zikagonga mwamba kufuatia kufikia maeneo ya kina kirefu cha ziwa.
Hata hivyo Sendiga alimuomba Waziri kuongeza nguvu zaidi ya Kifedha kutoka wizarani ili kupata teknolojia sahihi zaidi itakayosaidia kuharakisha zoezi hilo na kulinusuru ziwa Babati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...