
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi,akizungumza kwenye hafla ya utoaji tuzo kwa vijana chipukizi iliyoandaliwa na Taasisi ya TEYA,iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi,akiwa katika picha ya pamoja wakati hafla ya utoaji tuzo kwa vijana chipukizi iliyoandaliwa na Taasisi ya TEYA,iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, amesema serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kubuni mikakati ya kuhakikisha vijana wanapata fursa za kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza Novemba 16, 2023 jijini Dar es salaam kwenye hafla ya utoaji tuzo kwa vijana chipukizi iliyoandaliwa na Taasisi ya TEYA, Mhe.Katambi amesema fursa hizo ni pamoja na kuwapatia mafunzo ya ujuzi na stadi za kazi kupitia programu ya Ukuzaji Ujuzi.
“Serikali inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira wezeshi ili kuwawezesha vijana walio katika sekta isiyo rasmi na wahitimu wa vyuo kuweza kujiajiri kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya uzalishaji mali hasa kilimo,”amesema.
Aidha, amesema ili kuhakikisha kuwa vijana wanapata mitaji, Serikali imeboresha Mwongozo wa Utoaji Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) ambapo kwa sasa kijana mmoja mmoja anaweza kukopa.
“Niwashukuru waaandaaji wa tuzo niahidi serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote ambao wanatoa motisha kwa vijana na kuwahamasisha katika kuendeleza vipaji vyao,”amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...