Na Mwandishi Wetu


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameipongeza Benki ya Mandeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa mchango wake katika kutoa mikopo yenye riba nafuu na hivyo kuchangia kuboresha maisha ya wakulima na kukuza uchumi wa nchi ambao kwa kiasi kikubwa unategemea kilimo.

Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo kwa TADB wakati alipokuwa akitembelea Maonesho ya Huduma za Kifedha yanayoendelea jijini Arusha.


Alisema, Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na benki hiyo katika kuleta mageuzi kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima wa Kitanzania na kuitaka kuendelea hivyo hivyo.


Katika hotuba yake ya ufunguzi wa maonesho hayo, Majaliwa alizitaka benki za biashara nchini kufikiria kupunguza viwango vya riba ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kukopa kwa urahisi na kufanya shughuli zitazowaingizia kipata.

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano na Masoko wa TADB Amani Nkurlu

Alisema kauli ya Waziri Mkuu inaipa benki hiyo nguvu zaidi ya kuendelea kuwahudumia wakulima hapa nchini.


“TADB ipo mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wakulima wanapata mikopo yenye riba na masharti nafuu. Benki tayari imeshashusha viwango vya riba kwa mikopo inayotoa kwa wakulima hadi kufikia asilimia 9,” alisema.

Ili kuhakikisha kuwa wakulima wanapata fursa zaidi za kimikopo, alisema TADB imeboresha Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wakulima Wadogo (SCGS) na kufafanua kuwa mfuko huo sasa unauwezo wa kutoa dhamana ya hadi asilimia 70 kwa mikopo inayoombwa na wakulima.


“Tunaami kuwa hatua hii itaongeza hamu kwa taasisi za fedha ambazo ni washirika wetu kuutumia mfuko huu na hivyo kuongeza idadi ya wakulima ambao ni wanufaika,”alisema 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakati alipokuwa akitembelea maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayofanyika jijini Arusha.

Susan Kiwia (kushoto) mfugaji wa kuku wa nyama na mayai kutoka Ariana Poultry Arusha na mnufaika wa mikopo ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) akifafanua jambo kwa wananchi waliotembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayofanyika jijini Arusha.
Sophia Sokoni, Afisa maendeleo ya biashara kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) akifafanua jambo kwa wakina mama kutoka jamii ya wafugaji waliotembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayofanyika jijini Arusha.

Faithful Joshua, Afisa huduma kwa wateja kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) akifafanua jambo kwa mwananchi aliyetembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayofanyika jijini Arusha.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...