*Ni katika uwasilishwaji wa hesabu zinazokidhi viwango vya NBAA

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) yangara nafasi ya kwanza kwa Mashirika ya Umma ya Udhibiti katika uandaaji bora wa Hesabu mwaka 2022.

Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).

TASAC tangu ilipoanzishwa imekuwa ikishikiria nafasi mbalimbali katika Tuzo hizo za NBAA

TASAC imeshika nafasi ya kwanza ya uwasilishwaji bora wa hesabu mwaka 2022 ikishindanishwa na mashirika mengine ya Umma ya Udhibiti wakitumia viwango vya kimataifa vya kutayarisha hesabu

Akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Fedha TASAC Pascal Karomba amesema ushindi huo umewapa chachu ya kuendelea kuboresha utendaji wake katika maeneo wanayosimamia na utoaji wa huduma bora zinazokidhi viwango wa ndani na nje ya nchi.

“Ushindi huu unatoa ujumbe wananchi kuwa tunanachosimamia kipo salama na fedha zao hakuna zilizopotea na tutaongeza nguvu zaidi kuhakikisha tunakuwa kioo bora kwa wananchi,mtu sasa akiagiza mbolea au mchele kutoka nje kupitia bandari zetu awe na uhakika itafika salama” alisema.

Amesema shindi huu si wa mara ya kwanza kwa Shirika kuibuka kidedea na kufanya kuendelea kujiweka imara zaidi.

Karomba amesema mafanikio hayo yameendelea kuchochea kuimarika kwa utendaji ndani ya taasisi hiyo.

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar Jamal Kassim Ali akimkabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza katika kipengele cha Taasisi za Udhibiti wa Umma Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Pascal Karomba katika hafla ya utoaji wa Tuzo za NBAA jijini Dar es Salaam.
 

Mkurugenzi wa Fedha wa TASAC  Pascal  Karomba akiwa katika picha na wafanyakazi wa TASAC kwenye tuzo za NBAA jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...