Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) imeibuka mshindi wa tatu kwa uandaaji na uwasilishaji bora wa hesabu za mwaka kwa 2022 uliozingatia viwango vya taifa na kimataifa vya uhasibu katika tuzo zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).

Tuzo hizo zimekabidhiwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe,CPA Jamal Kassim Ali, usiku wa Desemba 1, 2023 katika ukumbi wa Hoteli ya APC Bunju Jijini Dar es Salaam,wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wahasibu na Wakaguzi ambao hushindanisha ubora katika uandaaji na uwasilishaji wa  taarifa za hesabu za mwaka uliozingatia viwango vya kitaifa na kimataifa vya Uhasibu.

Jumla ya Taasisi 98 ambazo ziliwasilisha hesabu mwaka 2022 ziligawanywa katika makundi 18 ambapo Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania walifanikiwa kuibuka mshindi wa tatu katika kundi lake kipengele cha Taasisi za serikali kuu zilizoandaa kwa ubora hesabu za mwaka 2022, huku nafasi ya pili ikishikwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) na nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (TRO).

Mkutano mkuu wa mwaka wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) hufanyika kila mwaka ambapo taarifa za hesabu kwa Serikali, Taasisi na Mashirika huwasilishwa kwa bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi kisha bodi huchagua  kundi la wataalam wabobezi na kukagua ubora wa uwasilishwaji kwa kuangalia kama viwango vya kitaifa na kimataifa vimezingatiwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...