Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kampeni yake ya msimu wa Sikukuu za mwisho wa mwaka inayofahamika kama "Tabasamu Tukupe Mashavu," ikilenga kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu, vocha za manunuzu na punguzo la bei kwenye huduma mbalimbali za kijamii na manunuzi ya vifaa vya kielectorinic. Kwa kampeni hiyo, inalenga kutoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kufurahia pamoja na wapendwa wao wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki.


Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo ilifanyika mapema leo makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo kampuni washirika wa kampeni hiyo kama Samsung, Auto Express, AG Energies, PUMA, Samaki Samaki, ABC Emperio na wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo na Wakubwa wa benki hiyo, Bw Elibariki Masuke.

“Jina la kampeni, “Tabasamu Tukupe Mashavu,” linakwenda sambamba kiini cha msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, ambapo “Tabasamu” inaashiria furaha inayotokana na uwezo wa kufanya miamala na malipo popote ulipom huku “Mashavu” ni pale unapopata huduma nzuri na za kuridhisha tena kwa kurudishiwa thamani zaidi . Kimsingi kampeni hii imebuniwa ili kuwahamasisha wateja wetu kushiriki furaha ya miamala na marafiki, familia, na wapendwa wao katika kipindi hiki cha sikukuu, wakiwa na uhakikisho kwamba NBC iko tayari kuwaunga mkono kwa kutoa zawadi za kuvutia. ’ Alieleza Masuke

Kwa mujibu wa Masuke katika kipindi chote cha kampeni hiyo ya mwezi mmoja, wateja wa benki hiyo watakuwa kwenye nafasi kufurahia upendeleo wenye kuvutia kwenye maeneo mbalimbali kama vile maduka, supermarkets na mtandaoni.

“Zaidi wateja wetu watakuwa kwenye nafasi zawadi mbalimbali kama vile smart TV ZA Samsung, simu janja za Samsung Galaxy Z-Flip 4, na Vocha za kufanya manunuzi zenye thamani ya hadi Tsh 500,000. Pia mawaka wetu na wateja wetu wenye mashine za malipo ya NBC (POS) wanazi nafasi za kujishindia pesa taslimu’’ Alisema.

Alisema ili kushiriki kwenye kampeni hiyo wateja wa benki hiyo wanatakiwa kutumia kadi zao za NBC VISA kufanya miamala kwenye mashine za ATM, Wakala, maduka, vituo vya mafuta,baa, migahawa, Airbnb, safari, hoteli na malipo mbalimbali ya mtandaoni kama vile Netflix, Amazon, na usajili wa mtandaoni.

"Tunataka kugeuza kila shughuli kuwa sherehe msimu huu wa sikukuu kupitia kampeni hii ya 'Tabasamu Tukupe Mashavu'. Kutumia Kadi yako ya NBC VISA kunafungua milango ya ulimwengu wa zawadi. Iwe unafanya ununuzi, unakula, unajaza mafuta kwenye vituo vya mafuta, au kufurahia wakati wako huku ukiwa umekaa kwa utulivu katika Airbnb au hoteli, kila ‘unapochanja’ unazidi kujileta karibu na zawadi za kusisimua kama ikiwemo kurudishiwa pesa taslimu na mapunguzo ya bei kwenye huduma za washirika wetu ." Aliongeza.

Masuke alitumia fursa hiyo kuwasisitiza wateja wa benki hiyo kutumia huduma za NBC Kiganjani, ATM, na NBC Wakala kulipa kufanya miamala na kutuma fedha kwa wapendwa wao katika msimu huu wa sikuu.

Kwa upande wao kampuni wadau wa kampeni hiyo wakiwemo Samsung, Auto Xpress, AG Energies, Samaki Samaki, na ABC Emperio walisisitiza dhamira yao kupunguza bei kwenye bidhaa zao ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao kwenye kampeni hiyo lengo likiwa ni kutoa unafuu kwa wateja wa benki ya NBC kupata fursa ya kufurahia sherehe za mwisho wa mwaka sambamba na wapendwa wao.


Mkurugenzi wa Idara ya Wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC, Bw Elibariki Masuke (Katikati) sambamba wawakilishi wa kampuni za Samsung, Auto Express, AG Energies, Samaki Samaki, ABC Emperio ambao ni wadau wa benki hiyo wakizindua kampeni ya pamoja ya msimu wa Sikukuu za mwisho wa mwaka inayofahamika kama "Tabasamu Tukupe Mashavu," inayotoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kufurahia pamoja na wapendwa wao kupitia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu, vocha za manunuzu na punguzo la bei kwenye huduma mbalimbali za kijamii na manunuzi ya vifaa vya kielectorinic
Mkurugenzi wa Idara ya Wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC, Bw Elibariki Masuke (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya msimu wa Sikukuu za mwisho wa mwaka inayofahamika kama "Tabasamu Tukupe Mashavu," inayotoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kufurahia pamoja na wapendwa wao kupitia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu, vocha za manunuzu na punguzo la bei kwenye huduma mbalimbali za kijamii na manunuzi ya vifaa vya kielectorinic. Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Biashara ya simu Tanzania kampuni ya Samsung Bw Mgope Kiwanga, Mkuu wa Idara huduma za benki Kidigitali NBC Bw Ulrik Peter (wa pili kushoto) na Meneja Masoko na Uhusiano wa Migahawa ya Samaki Samaki Bi Azmina Mohamed (Kushoto)





Mkurugenzi wa Idara ya Wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC, Bw Elibariki Masuke (wa pili kushoto) sambamba wawakilishi wa kampuni wadau wa benki hiyo , Mkuu wa Idara ya Biashara ya simu Tanzania kampuni ya Samsung Bw Mgope Kiwanga (wa pili kulia), Mkuu wa Idara huduma za benki Kidigitali NBC Bw Ulrik Peter (kulia) na Mkuu wa Idara ya wateja wakubwa na wadogo wa kampuni ya AutoExpress Bw Erick Munene (Kushoto) wakionyesha baadhi ya zawadi zinazousishwa kwenye ya msimu wa Sikukuu za mwisho wa mwaka inayofahamika kama "Tabasamu Tukupe Mashavu," inayotoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kufurahia pamoja na wapendwa wao kupitia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu, vocha za manunuzu na punguzo la bei kwenye huduma mbalimbali za kijamii na manunuzi ya vifaa vya kielectorinic.






Mkuu wa Idara ya Biashara ya simu Tanzania kampuni ya Samsung Bw Mgope Kiwanga (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya msimu wa Sikukuu za mwisho wa mwaka inayofahamika kama "Tabasamu Tukupe Mashavu," inayotoa fursa kwa wateja wa benki ya NBC kufurahia pamoja na wapendwa wao kupitia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu, vocha za manunuzu na punguzo la bei kwenye huduma mbalimbali za kijamii na manunuzi ya vifaa vya kielectorinic. Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC, Bw Elibariki Masuke (wa pili kushoto), Mkuu wa Idara huduma za benki Kidigitali NBC Bw Ulrik Peter (kushoto), Mkuu wa Idara ya wateja wakubwa na wadogo wa kampuni ya AutoExpress Bw Erick Munene (Kulia) na Kiongozi wa timu ya Mauzo ya Kampuni ya AG Energies Bi Ester Golan (wa pili kulia)


Kiongozi wa timu ya Mauzo ya Kampuni ya AG Energies Bi Ester Golan (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya msimu wa Sikukuu za mwisho wa mwaka inayofahamika kama "Tabasamu Tukupe Mashavu," inayotoa fursa kwa wateja wa benki ya NBC kufurahia pamoja na wapendwa wao kupitia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu, vocha za manunuzu na punguzo la bei kwenye huduma mbalimbali za kijamii na manunuzi ya vifaa vya kielectorinic. Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Biashara ya simu Tanzania kampuni ya Samsung Bw Mgope Kiwanga (Kushoto), Mkuu wa Idara ya wateja wakubwa na wadogo wa kampuni ya AutoExpress Bw Erick Munene (Kulia).


Mkuu wa Idara ya wateja wakubwa na wadogo wa kampuni ya AutoExpress Bw Erick Munene akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya msimu wa Sikukuu za mwisho wa mwaka inayofahamika kama "Tabasamu Tukupe Mashavu," inayotoa fursa kwa wateja wa benki ya NBC kufurahia pamoja na wapendwa wao kupitia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu, vocha za manunuzu na punguzo la bei kwenye huduma mbalimbali za kijamii na manunuzi ya vifaa vya kielectorinic. Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.



Meneja Mauzo wa Kampuni ya ABC Emperio Bw Ramadhani Mshana akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya msimu wa Sikukuu za mwisho wa mwaka inayofahamika kama "Tabasamu Tukupe Mashavu," inayotoa fursa kwa wateja wa benki ya NBC kufurahia pamoja na wapendwa wao kupitia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu, vocha za manunuzu na punguzo la bei kwenye huduma mbalimbali za kijamii na manunuzi ya vifaa vya kielectorinic. Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko na Uhusiano wa Migahawa ya Samaki Samaki Bi Azmina Mohamed akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya msimu wa Sikukuu za mwisho wa mwaka inayofahamika kama "Tabasamu Tukupe Mashavu," inayotoa fursa kwa wateja wa benki ya NBC kufurahia pamoja na wapendwa wao kupitia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu, vocha za manunuzu na punguzo la bei kwenye huduma mbalimbali za kijamii na manunuzi ya vifaa vya kielectorinic. Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam

“Jina la kampeni, “Tabasamu Tukupe Mashavu,” linakwenda sambamba kiini cha msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, ambapo “Tabasamu” inaashiria furaha inayotokana na uwezo wa kufanya miamala na malipo popote ulipom huku “Mashavu” ni pale unapopata huduma nzuri na za kuridhisha tena kwa kurudishiwa thamani zaidi . Kimsingi kampeni hii imebuniwa ili kuwahamasisha wateja wetu kushiriki furaha ya miamala na marafiki, familia, na wapendwa wao katika kipindi hiki cha sikukuu, wakiwa na uhakikisho kwamba NBC iko tayari kuwaunga mkono kwa kutoa zawadi za kuvutia.’’ - Elibariki Masuke, Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC.

Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo ilifanyika mapema leo makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo kampuni washirika wa kampeni hiyo kama Samsung, Auto Express, AG Energies, Samaki Samaki, ABC Emperio na wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo na Wakubwa wa benki hiyo, Bw Elibariki Masuke (Katikati).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...