MWENYEKITI wa  Umoja wa wanawake Tanzania UWT, Mary Chatanda, leo Desemba 16, 2023 amezindua Kamati  ya  Mapambano dhidi ya ukatili wa Wanawake na Watoto.
Akizindua kamati hiyo katika Viwanja  vya Mnazi Mmmoja Jijini  Dar es Salaam  leo, Bi Chatanda amesema uundwaji wa kamati  hii ni kutokana na Maelekezo  ya Mh. Rais Dkt.  Samia Suluhu Hassan  katika hotuba yake kwenye mkutano  wa UWT Dodoma.
"Majukumu  ya kamati  hii ni kuweka Mikakati ya kushughulikia na kutokomeza vitendo vya ukakatili uzalilishaji kwa  wanawake na watoto kama vile ubakaji na ulawiti." Amesema Chatanda
Pia ametoa maelekezo  kwa kuhakikisha mikoa inaunda kamati ya Mapambano dhidi ya ukatili kwenye  ngazi zote za Uongozi na kupanga Ratiba ya Viongozi wa UWT kutembelea madawati  ya jinsia na kuhakikisha taarifa ya kesi za ukatili na hatua zilizofikia zinawasilishwa makao makuu.
Amesema  pia kamati hiyo itaweza kuishauri kamati ya msaada wa kisheria kesi ambazo zinahitaji msaada wa kisheria kutoka UWT.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...