Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dkt. Amos Nungu akizungumza na watafiti, mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi walioshinda kwa kufanya tafiti bora. Hafla ya kukabidhiwa zawadi hiyo imefanyika hivi karibuni katika ukumbi wa COSTECH jijini Dar es salaam


WATIFITI nchini wamehimizwa kufanya tafiti zitakazokuwa suluhisho kwa changamoto na matatizo mbalimbali katika jamii

Wito huo umetolewa leo Desemba 14 na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Utafiti nchini (Costech), Dk. Amos Nungu alipokuwa anatoa zawadi kwa watafiti walioshinda kwa kufanya tafiti bora .

Amesema miaka mitatu iliyopita walishindanisha watafiti kutoka Chuo cha Kilimo cha Sokoine SUA na Chuo cha Mandela ambao walipata fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 1 ambayo ni sawa na Sh bilioni mbili kwa kila taasisi kwa ajili ya kufanya utafiti .

Amesema kuwa jukwaa hilo litaupaisha utafiti wa watafiti katika nchi zinazoungana katika baraza na utafiti la nchi 17.

"Safari hii tumepata Jukwaa lilelile na kwamba tunanchi 17 katika baraza la utafiti na tunawatafiti mbalimbali mfano utafiti wa SUA anayeangalia usalama wa chakula kwa hiyo kuna uwezekano ule utafiti ukawa suluhisho kwenye nchi nyingine mfano Ghana ,Congo au Zimbwabwe ambao ni washirika kwenye hili baraza"

Amewahimiza wafanye utafiti utakaotoa suluhisho kwenye jamii mfano kukausha dagaa Tanzania wakavuna dagaa Malawi kupitia Ziwa Nyasa kwa hiyo inawezekana matokeo yake mpaka Malawi wakaomba huo utafiti kwa hiyo hii ni fursa ya kujiuza kwa sababu utafiti wao utakwenda kujadiliwa kwenye nchi 17.

Dk. Nungu amesema kuwa utafiti utafanywa na taasisi nne kwa kuzingatia usawa wa jinsia ambapo watafiti wengi ni wanawake.

Kati ya taasisi 32 za kitafiti zilishindanishwa ni taasisi nne pekee ndizo zilizoshinda na kila mtafiti anapewa Sh milioni 120 kwa ajili ya kutekeleza utafiti huo na kwamba fedha hizo zimetolewa na Serikali ya Uengereza.

Mtafiti Mwandamizi katika Ofisi ya Utafiti wa uvuvi Tanzania, Alistida Mwijage amesema wamepokea tuzo kutoka kwa Costech ili kuendeleza utafiti wao unaohusu kupunguza upotevu wa dagaa kwa kutumia nishati ya jua.

Amesema kuwa katika utafiti huo wanakwenda kuboresha uvumbuzi ambao ofisi yao washaufanya siku za nyuma katika ziwa Tanganyika.

"Tulikuja na SolarTent inayoweza kukausha samaki kwa wepesi na umakini katika majira yoyote iwe ya mvua au jua tutatumia huo uvumbuzi kuhakikisha unatumika Pwani kwa sababu kuna dagaa wakubwa wanaoendana na wale wa Ziwa Tanganyika"

Amesema kuwa uboreshaji wa mfumo huo utawashirikisha wavuvi wa maeneo husika ili kuzidisha usanifu.

"Tutakwenda kuiboresha kwa kushirikiana na jamii ya wavuvi ambao ni wachakataji".

Amesema kuwa wachakataji wakubwa wa samaki ni wanawake hivyo uvumbuzi huo utawasaidia kukuza kipato na kuwa na uhakika wa ajira.

"Wachakataji wakubwa wa dagaa ni wanawake kwa hiyo kwa kufanya hivyo tunakwenda kukuza kipato cha kina mama kwa kuzalisha dagaa bora wenye kuuzika kwa bei nafuu pia tunawongea uhakika wa ajira." amesema.

Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA), Felix Nandonde amesema kuwa wao kama Chuo cha kilimo wameshiriki kwenye utafiti ambao ni kulipa thamani zao la Mbaazi kwa kutengeneza uji wa chap chap na Tambi.

Utafiti wao unalenga kwenda kupambana na utapiamlo au unyafuzi ama kwashakoo kwa watoto chini ya miaka mitano kwani asilimia 34 sawa na watoto milioni 3.3 wanachangamoto ya udumavu .

Amesema kwa kuwa Mbaazi zina Protini kwa hiyo wakitengeneza uji na tambi wataleta mabadiliko kwa sababu watoto watakunywa uji ambao una kiasi kikubwa cha protini

Amesema kuwa bidhaa hizo zitakuwa bei rahisi "kama mnavyojua Mbaazi zinauzwa bei ya chini kuliko mazao mengine tunaamini kwa utafiti huu tutakubaliana na changamoto ya udumavu".

Amesema kuwa bidhaa hizo zitasambazwa na kampuni ya Tanya.

Dk. Mohammed Dhamir Kombo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kilimo Zanzibar aliyeiwakilisha Tume ya Mipango ya Zanzibar kwa ajili ya kushiriki makabidhiano ya tuzo ya kutekeleza tafiti .

Amesema kuwa upande wao wamefanya utafiti juu ya vikwazo vinavyolirejesha nyuma zao la Karafuu visiwani Zanzibar na kupendekeza mikakati ya kuendeleza zao hilo.

"Lengo kubwa ni kuongeza uzalishaji na thamani itakayopelekea kuongeza pato la nchi ya Zanzibar"

Amesema kuwa uzalishaji wa zao hilo umepungua ukilinganishwa na miaka ya nyuma.

"Kwa sasa uzalishaji umepungua kwani miaka 150 iliyopita Zanzibar ilikuwa ikizalisha takribani tani 38,000, mfano mwaka 1830 lakini sasa hivi uzalishaji umekuwa tani 8,000 tu unaweza ukaona namna ilivyoporomoka" amesema Dk. Mohammed.

Amesema kuwa uzalishaji huo wa tani 8736 umeingizia nchi ya Zanzibar kiasi cha Sh bilioni 144.9 kwa mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...