NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOSHI

KAIMU Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Jairy Khanga, amesema madaktari wanaofanya Tathmini za Ulemavu na Magonjwa yatokanayo na Kazi, wanapaswa kufanya kazi hiyo kwa uadilifu ili wanaostahili waweze kupata fidia stahiki na kwa wakati.

Dkt. Khanga, ameyasema hayo Desemba 8, 2023, wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya Tathmini za Ulemavu na Magonjwa yatokanayo na Kazi kwa madaktari wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini inayojumuisha Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara na kufanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mjini Moshi.

“Sisi tukiwa watarajiwa wa fidia, lazima tuhakikishe haki inayotakiwa kutolewa kwa mwenzetu ambaye amepata ajali kwa bahati mbaya au ameugua kutokana na mazingira ya kazi yake, basi twende tukaifanye kazi hiyo kwa weledi mkubwa.” Amefafanua Dkt. Khanga.

Amesema matarajio ya WCF lakini pia Serikali, ni kuona mafunzo waliyopata washiriki yanawasaidia kufanya tathmini uhakika ambayo haina mgongano wa maslahi kwa mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu. 

Vilevile ni matarajio ya mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na kazi, kuwa atapata fidia anayostahili bila manung’uniko, amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini, WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, amesema, Mfuko umepanua wigo wa kutoa mafunzo ya Tathmini za Ulemavu na Magonjwa yatokanayo na Kazi kwa Madaktari kuanzia ngazi ya Vituo vya Afya hadi Hospitali za Rufaa za Kanda.

“Kama alivyosema Mkurugenzi Mkuu wakati wa ufunguzi wa mafunzo haya, lengo letu ni kwamba, kila mfanyakazi, mahali popote alipo, endapo ataumia au kuugua kutokana na kazi, apate fidia stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.” Amesisitiza Dkt. Omar.

Amesema, Mafunzo hayo yanawawezesha madaktari kupata uelewa wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini sahihi ili hatimaye mlengwa apate anachostahili, bila kumzidishia au kumpunguzia.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wengine, Dkt. Kisse Kamwela, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwekeza kwenye Mfuko na hivyo kuweza kutekeleza majukumu yake ikiwemo kutoa elimu ya fidia kwa makundi mbalimbali, madaktari wakiwemo.

“Mimi kama Mfanyakazi, ninanufaika na Mfuko huu, mafunzo haya yameniwezesha kujua haki zangu kama mfanyakazi, lakini kama daktari nimejifunza namna ya kumuhudumia mgonjwa aliyepata changamoto kutokana na kazi” amesema.

Baadhi ya Madaktari wa Kanda ya Kaskazini, wakionyesha stika za utambulisho wa Huduma za WCF, watakazobandika kwenye maeneo yao ya kazi.
Baadhi ya madaktari wa Kanda ya Kaskazini, wakiwa kwenye mafunzo.
KAIMU Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Jairy Khanga, akizungumza na madaktari.
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini, WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Jairy Khanga (katikati), akipongezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini, WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, baada ya kuongea na madaktari wa Kanda ya Kaskazini. Anayeshuhudia ni Mhadhiri Mwandamizi kutoka MUHAS, ambaye ndiye Mwenyekiti wa Jopo la Wataalamu wa mafunzo hayo, Dkt. Robert Mhina.
 
Afisa Tathmini Mwandamizi, WCF, Dkt. Kyangwe Wambura (kushoto), akizungumza na baadhi ya washiriki wa mafunzo.
Afisa Tathmini Madai, WCF,  Dkt. Matilda Rusibamayila, akitoa mada wakati wa mafunzo hayo. 
Afisa Tathmini Madai, WCF, Dkt. Fransisxavery Chila, akielekeza namna ya kutumia baadhi ya vifaa vya kupima kiwango cha ulemavu wakati wa mafunzo. Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...