Na Fauzia Mussa

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa huduma za Afya Yasin Ameir Juma amewataka wanachama wa Mfuko huo kuwa waaminifu ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

Akitoa elimu juu ya dhana ya kuanzishwa kwa mfuko huo kwa makamanda na wapiganaji wa kikosi maalum cha kuzuia magendo huko makao makuu ya KMKM Kibweni amesema mfuko wa huduma za Afya umeanzishwa kwa lengo la kuhakikisha Wananchi wote wanapata matibabu bora Nchini.

Alisema kuwa kwa hatua za awali mfuko umeanza kutoa huduma hizo kwa wananchama wake wa sekta rasmi katika hospitali binafsi na kuendeleza kupatiwa huduma kama hizo katika hospitali mbalimbali za Serikali ili kukamilisha adhma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya kutoa matibaabu bora kwa wote.

Amesema mfuko haukuweka ukomo wa usajili wa wawatoto wakuwazaa kwa wanachama wake ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wategemezi wa walio chini yao.

Katika kupunguza msongamano wa wagonjwa mfuko umeanza kutoa huduma kupitia vituo 30 vya Serikali na binafsi na wanaendelea kupokea maombi ya kutoa huduma kwa wananchi kutoka vituo vyengine ili kuimarisha huduma za afya Nchini.

Hata hivyo alisema mfuko umejipamga na kupambana na udanganyifu wa aina yoyote na kuwasihi wanachama wake kuwa waaminifu wakati wanapotumia mfuko huo na kusema kuwa wakati wote wataingia makubaliano na NHIF ili kuhakikisha wanachama wake wanapata matibabu wakiwa nje ya Zanzibar.

Mkuu wa Utawala KMKM Captain Fadhil Ramadhan Mberwa amesema miongoni mwa matunda yanayopatikana kupitia mfuko huo nikuweza kupata huduma za afya pale ambapo huwezi kugharamia matibabu hayo binafsi na wategemezi wako.

Aidha aliitaka jamii kuwa waaminifu na kutokufanya uhujumu katika mfuko huo ili kuisaidia Serikali kudumisha na kuendeleza kwa maslahi ya taifa pamoja na kuwataka kufiksha elimu hiyo Kwa jamii ili kuwajengea uelewa juu ya dhana ya mfuko huo.

"Endapo tutafanya udamganyifu itakua tuaniibia Serikali"alisema Mkuu huyo

Nao maafisa na wapiganaji hao waliwaomba watendaji wa mfuko huo kutoa elimu ya kutosha kwa jamii juu ya Rufaa,vituo na hospitali zinazotoa huduma kupitia mfuko huo ili kuepusha usumbufu wakati wa kutafuta huduma hizo.


 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa huduma za Afya Yasin Ameir Juma akijibu baadhi ya maswali ya  wapiganaji wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo juu ya dhana ya  mfuko wa huduma za Afya huko makao makuu ya KMKM  Kibweni Zanzibar.
 

Afisa Masoko na Uhusiano Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar Asha Kassim Biwi akizungumza na makamanda na  wapiganaji wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo juu ya sheria iliyoanzisha mfuko wa huduma za Afya huko Makao Makuu ya KMKM Kibweni Zanzibar.
 

Mkuu wa Utawala Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo KMKM Captain Fadhil Ramadhan Mberwa akizungumza machache na kuurabisha ujumbe kutoka mfuko wa Huduma za Afya kutoa elimu kwa makamanda na  wapiganaji wa katika makao makuu ya KMKM  Kibweni Zanzibar.
Mpiganaji wa Kikosi cha Kuzuia Magendo Mussa abdul-kadri Ali akiuliza maswali kwa Maafisa wa Mfuko wa huduma za Afya wakati wakipatiwa elimu juu ya dhana ya mfuko huo huko makao makuu ya KMKM Kibweni Zanzibar.

Mpiganaji wa Kikosi cha Kuzuia Magendo Iddi Vuai Haji  akiuliza maswali kwa Maafisa wa Mfuko wa huduma za Afya wakati wakipatiwa elimu juu ya dhana ya mfuko huo huko makao makuu ya KMKM Kibweni Zanzibar.

 

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...