News
Njombe

Kamati ya siasa mkoa wa Njombe imeagiza ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe kuhakikisha inatoa fedha kwa wakati ili kukamilisha maboma ya miradi mbalimbali iliyojengwa kwa nguvu za wananchi na kukwama kutokana ukosefu wa fedha inayosubiriwa kutokana na kufungwa kwa mifumo ya serikali ya utoaji wa fedha.

Katibu wa Siasa na Uenezi mkoa wa Njombe Josaya Luoga ametoa agizo hilo baada ya kamati ya siasa kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Zahanati ya kijiji cha Itipula lililopo kata ya Ihanga lililojengwa kwa nguvu ya wananchi mpaka hatua ya bimu na kusimama ikisubiriwa fedha kutoka halmashauri ili kuendelea na ujenzi ambapo Luoga amesema halmashauri hiyo imekuwa na maboma mengi yaliyokwama kutokana na mfumo.

"Mifumo ikifunguka tunataka wananchi wapate hiyo fedha kwa wakati na niaweleze wananchi ni kweli kwamba kuna changamoto kwa muda wa miezi mpaka mitatu sasa kwenye mifumo kufunguka,kwa hiyo mimi niwaombe halmashauri fedha ikifunguka leteni fedha kwa wananchi"amesema Luoga

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Grewin Mtulo ambaye ni afisa mtendaji wa kijiji cha Itipula amebainisha kuwa mpaka sasa ujenzi wa jengo la zahanati hiyo umefika hatua ya bimu kwa nguvu za wananchi ukiwa umeghalimu takribani shilingi Milioni ishirini na saba.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi,Daniel Mwasongwa ambaye ni mratibu wa jitihada za jamii amewaomba wananchi kuwa wavumilivu ambapo wanachokisubiri ni kufunguliwa kwa akaunti ya kupitisha fedha za serikali za maendeleo ambapo Shilingi Milioni hamsini zitatolewa ili kuendeleza ujenzi.

"Nchi nzima kwenye akaunti ya kupitisha fedha za serikali za maendeleo imefungwa,sasa lini itafunguliwa hatujui kwa hiyo ikifunguliwa hela zitakuja"amesema Mwasongwa

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Itipula akiwe Mario Mpogolo na Amoni Lipumbwe wameiomba serikali iweze kuwasaidia kukamilisha jengo hilo kutokana na nguvu kuwa waliyoitumia ili waweze kuanza kupata huduma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...