*Kutembea na bahasha ya kutafuta kazi sio kusudio kuandaliwa chuoni

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Serikali imesema kuwa wahitimu katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kuwa wabunifu kwa kutumia taaluma waliyoipata katika kujiajiri na kuwa mchango wa kiuchumi katika Taifa

Wahitmu jambo la kwanza kuona mbali fursa ya kujiajiri kwanza na kuajiriwa kuwa nafasi ya pili inawezekana na kutembea na bahasha ya yenye taarifa ili upate kazi huko ni kutumia ubunifu ambao umetokanao katika mwaka wa kwanza hadi unahitimu

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha Dkt.Mwiglu Nchemba katika Mahafali ya 21 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Dar es Salaam jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Elijah Mwandumbya amesema TIA ina wahadhiri wenye ujunzi ndio ulitumika hivyo ni fursa yenu wahitimu kwenda kutumia kuhudumia wananchi mbalimbali ikiwemo kufanya ujasiriamali.

"Wahitimu mmevuka mabonde na milima kwa wazazi kujitoa kwenu na changamoto nyingi ambazo ni zaidi ya milima mkavuka hivyo kazi kwenu ni kufanya kazi suala Kuwaajiri ni nafasi ya pili.

Mwandumbya amesema katika mahafali haya nimeona maonyesho ya ujasiriamali kwa wahitimu waliopita na wahitimu wapya hayo ni matokeo yanayoonyesha mnakwenda katika soko la ajira moja kwa moja.

Aidha amesema kuwa soko la ajira kwa umma ni 650000 ambazo zina watu hivyo kwa serikali haiwezi kuajiri watu wote ndio maana kuna sekta binafsi ambapo wahitimu ni sehemu kwenda kuwa waajiri miradi mlioanzisha kwenye sekta hiyo binafsi.

Naibu Katibu Mkuu Mwandumbya amesema TIA ni miongoni mwa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha ambayo Wizara inaitegemea katika majumu ya kutoa elimu bora na yenye ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi katika kutoa ushauri wa kitaalam na kufanya tafiti za kutatua changamoto halisi kwa jamii na Kampuni na Viwanda.

Nata hivyo amesema TIA ina mchango katika kuzalisha wataalam wabobezi kwenye Tasnia ya uhasibu,usimamizi wa fedha ,ununuzi na ugavi hivyo serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwaunga mkono kwa kuachangia maendeleo ya miundombinu ili watalaam hao waendelee kuzalishwa.


Mwandumbya ameitaka TIA kuweka mikakati ya kuhakikisha taarifa zinawafikia watanzania wote popote walipo ndani na nje ya nchi ili watumie fursa za kujiendeleza kielimu kupitia kozi mbalimbali, zinazotolewa kwenye Chuo.

Alisema kuwa Serikali imetumia gharama kubwa kujenga miundombinu hiyo, ikilenga kupunguza adha wakati wa uendeshaji wa shughuli za Taasisi na kuboresha utendaji na utoaji wa huduma kwa ujumla hasa katika kutoa elimu.

“Serikali inatumia fedha za watanzania kugharamia ujenzi wa miundombinu. Hakikisheni watanzania wanapata taarifa za utekelezaji wa miradi hiyo kila mara, pamoja na masuala mbalimbali yanayofanywa na Serikali kupitia Taasisi hii", amesema Mwandumbya.

Amesema miundombinu iliyojengwa iwekewe mikakati ya utunzaji ili idumu kwa kipindi kirefu huku ikibaki katika hali ya ubora wa kutoa elimu kwa watanzania wote.

Aidha aliwataka wahitmu wafanye kazi kwa bidii, uadilifu, ubunifu, umakini, weledi na kujiepusha na uzembe, huku wakifanya kazi kwa kuzingatia Sera, Sheria, Taratibu na Kanuni ili kujiimarisha zaidi na kuweza kushindana katika soko la ajira.

“Lazima muendelee kujielimisha kwa lengo la kujenga ujuzi na maarifa ya kutosha kwa vijana kadri inavyowezekana, ili muweze kutumikia taifa kwa viwango vya hali ya juu” amesema Mwandumbya.

Alifafanua kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na TIA kuhakikisha kuwa wanaweza kukabiliana na changamoto mbalimbali hasa zinazotokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia,pamoja na ongezeko la idadi ya wanachuo.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Prof. William Pallangyo, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya kusomea na kufundishia, katika kampasi za TIA kupitia Wizara ya Fedha.

Katika mahafali hayo wahitimu 7,222 wa kampasi ya Dar es Salaam, wakiwemo Wanawake 3,957 na Wanaume 3,269 walitunukiwa vyeti vya shahada mbalimbali.

Hata hivyo Wahitimu kwa kampasi zote sita ni 13,265, wakiwemo wanawake 7,155 na wanaume 6,110 isipokuwa kampasi ya saba ya Zanzibar ambayo imeanza kupokea wanafunzi mwaka huu.

Amesema kuwa chuo kimekuwa na masomo ya ujariamali lengo lake ni kuwajenga katika kwenda kujiajiri katika mawazo bunifu.

Prof.Pallangyo amesema kuwa wanafunzi wakiwepo chuoni wanajifunza vitu vingi kwa vitendo hiyo inakwenda kufuta kuwa na usomi wa nadharia.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara katika Taasisi ya Uhasibu Wakili Said Chiguma amesema kuwa katika ushauri TIA wamekuwa na uwezo wa kuanisha nadharia na vitendo ambapo wanafunzi wamekuwa wanaibua mawazo ya biashara hivyo wahitmu ni kazi kuendeleza ubunifu huo.

Amesema katika jitihada zao TIA kuendelea na lengo kuu la kuwajengea wanafunzi kuwa na tabia ya kujiajiri kwenye ujasirimali.
Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya akizungumza katika Mahafali ya 21 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
 

Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya akifurahi jambo na Mbunge wa Afrika Mashariki kundi la Vijana aliyehitimu shahada katika Mahafali ya 21 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
 

Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya akiwatunuku wahitimu kwenye  Mahafali ya 21 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
 

Picha ya Pamoja ya Naibu Katibu Mkuu Elijah Mwandumbya ,Mwenyekiti wa Bodi Wakili Said Chiguma ,Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA Prof.William Pallangyo na Mbunge wa Afrika Mashariki kwenye Mahafali 21 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)


Picha Mbalimbali katika mahafali 21 ya TIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...