Na Mwandishi wetu.

Serikali imesema kuwa hakuna mwananchi yoyote anayefukuzwa katika eneo la Loliondo lenye  ukubwa wa kilomita za mraba 2,500 ambalo lilimegwa kutoka pori la akiba Pololeti katika Wilaya ya Ngorongoro   ambalo Serikali ililitoa kwa ajili ya shughuli za wananchi.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma Msemaji  Mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo Bw.Mobhare Matinyi  amesema  taarifa hizo hazina ukweli wowote, kwani Serikali ilikabidhi eneo hilo kwa ajili ya matumizi ya Wananchi kufuatia kumegwa kwa lililokuwa  pori tengefu la Loliondo mwaka 2022.

Amebainisha kuwa awali pori hilo lilikuwa na   ukubwa wa kilomita  za mraba 4,000 ambapo baada ya kugawanywa Kilomita za mraba 1,500 ambazo ndio Pori la akiba pololeti  zilibaki kwa ajili ya shughuli za uhifadhi na Kilomita za Mraba 2,500 Serikali ilizitoa kwa ajili ya Wananchi kufanya shughuli zao za maendeleo.

Bw.Matinyi alisisitiza kuwa  serikali itaendelea kusimamia shughuli za uhifadhi katika eneo la Ngorongoro na kuwataka wananchi kupuuza taarifa hizo  kwa kuwa Serikali inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na kufuata misingi ya haki za binadamu.

Amewataka wananchi wote wanaoishi katika eneo walilopewa na  Serikali lenye kilomita za mraba 2500 kuendelea na shughuli zao na kupuuza taarifa hizo zenye lengo la kupotosha umma.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...