Na Mwandishi wetu.

Msemaji Mkuu  wa serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari -Maelezo  Bw.Mobhare Matinyi amesema serikali itaendelea kuheshimu haki za binadamu katika zoezi la kuhamisha watu wanaojiandikisha kuhama kwa  hiyari kutoka eneo la hifadhi ya Ngorongoro kwenda maeneo mengine nchini.

Matinyi ametoa kauli hiyo akizungumza na  Wanahabari jijini Dodoma kufuatia msimamo wa baadhi ya wabunge wa Bunge la Ulaya uliotolewa wiki hii kuhusu zoezi la kuhamisha wananchi wa Ngorongoro kwa hiari  ambapo Matinyi amesisitiza msimamo wa Serikali kuwa inawahamisha wananchi wanaojiandikisha wenyewe kuhama katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro na kwamba  hakuna  ukiukwaji wowote wa haki za binadamu unaofanyika katika utekelezaji wa zoezi hilo.

Ameeleza kuwa serikali ya Tanzania inatekeleza mpango huo  ikiamini katika kutimiza malengo ya dunia ya milenia ya kuhakikisha usalama wa watu wake, huduma bora za kijamii ikiwemo elimu, afya na maji huku akisema kwamba serikali itaendelea kuhamasisha wananchi hao kukubali kuhama kwa hiyari.

Bw.Matinyi ameeleza kuwa mtu yoyote au kundi linalotaka kutembelea eneo la  hifadhi ya Ngorongoro wanakaribishwa na wanachotakiwa kufanya ni kufuata taratibu ili waweze kuruhusiwa kwa kuwa Serikali haina sababu ya kumzuia mtu yeyote kufika eneo hilo.

Akizungumza hoja ya kuwepo kwa watu asili nchini Tanzania Bw.Matinyi amesema kuwa watanzania wote wanatambulika kwa utaifa wao ambapo kuna Zaidi ya makabila 120 na hivyo suala la kuhamisha watu katika hifadhi hiyo lisitazamwae katika kuhamisha kabila fulani bali wananchi wote waliopo huko wanahamisishwa kuhama kadri wanavyojiandikisha.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...