Na, Brow Jonas - WUSM
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema
Serikali itazindua Tuzo ya Kimataifa ya Kiswahili kwa Hayati Mwl. Julius
Kambarage Nyerere ili kuenzi mchango wake katika kukuza Kiswahili
duniani
Mhe. Ndumbaro amesema hayo leo Desemba 15, 2023 wakati wa
kongamano la 8 la Kiswahili lililoandaliwa na Chama Cha Ukuzaji
Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) Jijini Arusha.
Mhe. Ndumbaro amesema
tuzo hizo zitatolewa katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa
la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Ufaransa ikiwa ni heshima
ya Shirika hilo kuitambua lugha ya Kiswahili duniani na kutenga Julai 7
kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.
Ameongeza kuwa katika
tuzo pia watu wengine waliojitoa kukuza Kiswahili watatambuliwa na
kupewa tuzo kwa heshima ya Baba wa Taifa
Kongamano hilo
limehudhuriwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwemo
Ufaransa, Marekani, Malawi, Kenya na Uganda ambapo mijadala mbalimbali
ya kubidhaisha Kiswahili imejadiliwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...