Balozi wa Amani Dr.John Sushi ( kushoto) kikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa Compact Energies Ephraim Kimati tuzo ya Pacesetters Awards katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI ya usambazaji na ufungaji wa vifaa vinavyotumia umeme unaotokana na nishati ya jua, Compact Energies imeshinda tuzo ya utoaji huduma bora (Pacesetters Awards) iliyotolewa na Jubilant Stewards of Africa katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makampuni na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nje zimeshiriki tuzo hizo zenye lengo la kuchochea ukuaji kupitia sekta ya viwanda na biashara.
Akiongea baada ya kushinda tuzo hiyo, Meneja Masoko na Mauzo Fredy Pantaleo Msafiri amesema wanashukuru kupata tuzo hiyo, ikiwa ni matokeo ya kutoa huduma bora kwa wananchi kupitia umeme jua, ambao ni rahisi na rafiki katika utunzaji wa mazingira.
Pia ametoa wito kwa wananchi kutumia nishati hiyo ikiwa njia mbadala ya kupata nishati ya umeme yenye gharama nafuu na ya uhakika ili kujiletea Maendeleo.
Akiongea baada ya kushinda tuzo ya katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ambayo pia iliwahi kuwa washindi wa pili kwa utoaji huduma hiyo hapa nchini hivi karibuni Fredy Pantaleo Msafiri amesema nishati hiyo ni salama kwa matumizi na ni rafiki katika utunzaji wa mazingira.
Lakini pia amesema kuwa umeme jua ni wa uhakika, rahisi na ni endelevu, tofauti na nishati nyingine zinazoweza kukosekana kwa sababu ya changamoto mbalimbali.
”Dunia hivi sasa imebadilika na hakuna sababu ya kukaa giza au kushindwa na kushindwa kuzalisha huduma za viwandani kwa sababu ya ukosefu wa umeme,”
”Nchi zetu za ukanda wa Kusini mwa jangwa la Sahara zinapata jua la kutosha kwa muda mrefu, hivyo kuwa na nguvu kubwa ya kuzalisha nishati jua kwa matumizi ya nyumbani, ofisini na hata mashambani,”
”Uzuri wa gharama hii haulipii wakati unatumia, ukishafunga umefunga na upatokanaji wa huduma ni wa uhakika,”
”Tukiwa kampuni yenye uzoefu nchini katika kutoa huduma za umeme jua, tunawashauri wananchi kukimbilia nishati hii ambayo ni ya uhakika na salama ,”amesema Msafiri.
Amesema Tanzania inapiga kasi kubwa sana katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii kutokana na maendeleo ya ukuaji wa teknolojia.
Hivyo, ni bora jamii ikaenda sambamba na ukuaji wa teknolojia ili kukuza uchumi wa jamii na taifa kwa ujumla.
Katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kukuza uchumi nchini, amesema kampuni yake ya Kitanzania imewekeza katika matumizi ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma, hivyo ni vema nishati hiyo ikatumika mijini na vijijini katika shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato, ikiwemo sekta ya kilimo na umwagiliaji.
”Tukiwa kama kampuni ya Kizalendo, tunahakikisha huduma bora zaidi kwa Watanzania na ndio maana tumeweza kushinda tuzo mbalimbali sababu ya kutoa huduma bora kwa wananchi,”amesema.
Tuzo hizo zinazojulikana kama ’Pacesetters Awards’, zimetambua michango ya makampuni mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali duniani katika kuchochea ukuaji wa sekta ya viwanda.
Akiongea katika tuzo hizo zilizoandaliwa na Jubilant Stewards of Africa, Dr.John Shusho, mgeni rasmi Balozi wa Amani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesifu jitihada za makampuni mbalimbali katika kuleta mabadiliko ya uchumi kupitia ushindani wa kibiashara na utoaji huduma bora.
Ameyataka makampuni hayo kutumia ubunifu unaotokana na ukuaji wa teknolojia ili kuendelea kuwa na ushindani katika soko la dunia.
”Wakati tunafurahia maendeleo tuliyonayo, ni lazima tutambue kuwa uongozi bora hupelekea ukuaji wa uchumi kupitia uwajibikaji, uwazi na utoaji maamuzi sahihi,” amesema.
Pia ameyataka makampuni hayo kurudisha sehemu ya faida yao katika jamii, akisema kuwa ukuaji wa biashara haupimwi kupitia faida kubwa pekee, bali kupitia michango mbalimbali inayotolewa na makampuni hayo katika kuleta mabadiliko ya jamii.
Makampuni mbalimbali ya Tanzania yamepata tuzo hiyo likiwemo Shirika la Bima la Zanzibar na Raphael Logistics.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...