Na Fauzai Mussa, Maelezo Zanzibar
JAMII imehimizwa kudumisha usafi katika maeneo yao ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi juu ya suala la usafi katika Mji wa Zanzibar.

Akizungumza na wananchi wa shehia ya Mwera kwa kozi Mkuu wa Wilaya ya Kati Sadifa Juma Khamis amesema jukumu la kuweka usafi ni la kila mwananchi hivyo kila mmoja anawajibu wa kuweka usafi katika mazingira yaliyomzunguka.

Amesema zoezi la usafi si la baraza la mji pekee bali hata wananchi wana haki ya kusafisha pembezoni mwa maeneo yao na sehemu wanazofanyia harakati zao za biashara.

Hata hivyo aliwaomba wananchi wa Wilaya hiyo kuacha kutupa taka ndani ya mitaro na kuifanyia usafi mitaro hiyo mara kwa mara ili kuruhusu maji kupita na kuepuka athari zinazoweza kutokezea hasa katika kipindi hichi cha mvua.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Mji Kati Said Hassan Shaaban amesema ipo haja kwa jamii kuendeleza utaratibu wa kuweka usafi kwenye maeneo yao na kulifanya zoezi hilo kua endelevu.

Amesema ili kufikia adhma ya kuiweka Zanzibar katika hali ya usafi ni vyema taasisi zinazohusika na usafi wa mji kushirikiana na wananchi wa eneo husika kwa lengo la kuongeza nguvu na kuimarisha usafi katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.

Alifahamisha kuwa kujitolea kwa viongozi wa taasisi hizo katika kushiriki harakati za usafi kutahamasisha wananchi kuunga mkono agizo la Rais wa Zanzibar la kuhakikisha mji unakuwa safi..

Nao wananchi na wafanyabiashara wa eneo hilo na vijiji jirani wamelipokea agizo hilo na kuahidi kulifanyia kazi kwa kushirikiana na watendaji wa Baraza la Mji Kati.

Zoezi hilo la usafi limeratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kati pamoja na Baraza la Mji Kati na kushirikisha wadau, wafanyabiashara na wananchi wa shehia ya Mwera kwa kozi na Vijiji jirani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...