KAMPUNI ya iStore kupitia chapa ya simu aina ya iPhone wamefanya mazungumzo wadau wake juu ya bidhaa mpya ambazo wamezianzisha na hafla ya kuuaga mwaka 2023 katika hoteli ya Slipway Masaki Jijini Dar es Salaam, hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa semina fupi iliyoshirikisha wateja na watumiaji wa simu aina ya iPhone Mkurugenzi wa Kampuni ya iStore nchini Tanzania, Vipul Shaah amesema kukutana na wateja wao ni sehemu moja ya kufikisha elimu mbalimbali juu ya matumizi za simu za iPhone pamoja na kutambulisha bidhaa mpya zinazoingia sokoni.
"Nafasi hii ya kukutana na wateja wetu ni kuwapatia elimu jinsi gani wanaweza kutumia simu za iPhone pamoja na iPad ambazo mara nyingi zimekuwa zikileta mfumo mpya wa matumizi wa vifaa hivi, hivyo kukutana kwetu ni nafasi pekee mteja kufanya chaguo la bidhaa bora bila kuwepo kwa kizuizi cha kutofahamu kutumia programu au mfumo uliopo kwenye kifaa hicho."
Aidha Shaah ameongeza pia amesema wamezindua programu mpya itakayopatikana katika imac ambayo itakayopatikana kwa rangi 7 za kumvutia mteja.
Pia amesema matarajio yao makubwa kwa Wateja wao kueneza uelewa huo juu ya mifumo na programu zinazopatikana katika iMac na wapo tayari kuwapa bidhaa zilizo bora zaidi
Kwa upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya iStore Karigo amesema kuwa moja kati ya bidhaa hizo iPhone kwaajili ya mtanzania,
Pia amesema kuwa kampuni hiyo inamsadia mteja kuweza kubadilisha i Phone aliyonayo kwa kulingana na toleo ili kupata toleo jipya na la kisasa.
Akizungumzia kuhusiana na gharama amesema kuwa gharama za iPhone zao ni rahisi kabisa na ni iPhone ambazo ni toleo halisi (Original) kulingana na nchi ambapo zinatoka.
Ameongeza kuwa kwa wale waonunua simu katika kampuni yao wanauwezo wa kuipeleka simu kwaajili ya matengenezo pale inapoharibika ndani ya miaka miwili tangu kuinunua bila gharama yeyote.
Mkurugenzi wa Kampuni ya iStore nchini Tanzania, Vipul Shaah akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaama mara baada ya kutoa elimu kwa wateja wake.
Afisa Masoko wa Kampuni ya iStore Karigo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaama mara baada ya kutoa elimu kwa wateja wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...