•Nimejifunza kuwa na hazina kubwa ya watu kuliko Fedha (Dkt. Geordavie)
•Ukiwekeza kwenye mioyo ya watu utakumbukwa daima
Na.Vero Ignatus,Arusha
Wazazi na walezi wametakiwa kutokuwafanya watoto wao kama vikundi vya vikoba badala yake wawekeze Kwa watoto wao ili waweze kuwa mifano bora ya kuigwa na kuwasaidia wenzao
Hayo yamesemwa na Mtume Dastan Maboya wa kabisa la Calvary Assemblies of God katika ibada ya maziko ya aliyekuwa mtoto wa Nabii Mkuu wa Ngurumo ya Upako Dr GeorDavie ambaye pia alikuwa mzalishaji wa mziki wa bongo fleva na tamthilia mbalimbali,Nic Dave ambapo aliwataka familia pamoja na waombolezaji kukubali kuwa Nisher amefariki Dunia
Ibada ya maziko ya aliyekuwa mtoto wa Nabii Mkuu Dr.Geor Davie ,Nic Davie iliyofanyika leo Kisongo katika hema la Matamko Jijini Arusha, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwepo wa serikali , dini ,siasa , wasanii mbalimbali pamoja na wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi
Alibainisha wazazi wengi wamekuwa hawawekezi katika kuwapatia elimu watoto wao na ndio maana wamekuwa wakilalamika kuwa watoto wao hawawasaidi hiyo yote inatokana na kutowekeza katika kuwapa elimu watoto
"Najua kunamambo mengi yanasemwa lakini usiyasikiliza bali endelea kumuangalia yeye aliekuita na uendelee kumtumikia"alisema Maboya
Amesema tunajifunza kutoka Kwa mtumishi wa Mungu Ayubu kwamba alipoteza watoto wake saba lakini hakumuacha Mungu.
Alisema kuwa hakuna jaribu linaloweza kutoka kwenye familia ya mtu wa Mungu kama hajaupima uwezo, hivyo aliwataka waache Mungu abakie kuwa faraja yao maana Mungu anajua kwani Kila aina yeyote ya jeraha ni Mungu mwenyewe.
Alinikuu zaburi 34:8 alisema Mungu siku zote ndiye faraja ya kweli huku akimuuliza kwamba atazame tangia Mungu amemuita kwenye utumishi ni mambo mangapi Mungu amemvusha nayo? Hakuna wa kumtenga na Upendo wa Mungu.
Akizungumzia Nisher Mtume Maboyo kutoka 5:1- 35 amesema kuwa Mungu alimuelewa na akamjaza ujuzi na akili za moyoni Ili wapate kifundisha mara zote Mungu anaheshimu uzao wa tumbo la mtumishi wake.
Kwa upande wake askofu Mkuu wa makanisa ya ufunuo Joel Bendera alisema kuwa walio wa Mungu hawatikiswi na kitu chochote na kwakuwa yeye ni sauti ya Mungu asitikiswe na kitu chochote na kanisa hili haliwezi tikiswa na chochote ,pia alimpongeza Kwa namna amekuwa anasaidia serikali vijana wengi kupata ajira hivyo anastaili apongezwe.
Akitoa Salamu Kwa niaba ya serikali Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela alisema kuwa "Kwa niaba ya serikali Wanampa pole ambapo alifafanua kuwa Rais atakuja kimfariji pindi tu atakapokuja Arusha kwani anatambua umuhimu wake wa kufanya wananchi kuwa na amani'
Alifafanua kuwa amani ya watu wake ndio mafanikio ya serikali uwezi kuwa na sehemu ambayo watu wako wanapata amani ukaacha kuwa karibu nayo ,huku akisisitiza kuwa huduma ya Ngurumo ya Upako ni msaada mkubwa sana kwa serikali wanampa moyo na watamuunga mkono zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzo Ili aendelee kuwaunga mkono wataendelea kumuombea ili Mungu amvushe katika karibu hili.
Akizungumza Kwa niaba ya wasanii Ben Pole alisema kuwa watamkumbuka Nisher katika mambo mengi kwani ni kijana ambaye ameleta mapinduzi katika tasnia mzima ya mziki kwani kupitia yeye vijana wengi wameweza kujiajiri na kuajiri wengine.
Akizungumza mara baada ya kupokea Salamu za rambirambi Nabii Mkuu Dr.Geor Davie alisema kuwa mtoto wake amefariki katika umri wa miaka 34 amewaachia deni la kuwasaidia watu wenye umri wa miaka hiyo na kuendelea n anasikia sauti yake ikiwaambia vijana wanakulilia wasaidie hivyo atawasaidia amebainisha kuwa ,amejifunza kuwa watu ni azina muhimu kuliko fedha ,ukiwekeza Kwenye mioyo ya watu utakumbukwa daima
Alimallizia Kwa kuwataka vijana kutokata tamaa na kuwasihi fanyeni kazi Kwa bidii kwani Nisher alikuwa anafanya kazi kama anakufa kesho hivyo vijana wafanye kazi na yupo teari kuwasaidia.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...