MAKAMU Wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Philip Isdor Mpango amewataka watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii kwa maendeleo ya Taifa.

Amesema hayo leo Ikulu ya Chamwino, Dodoma wakati Rais Samia Suluhu Hassan akipokea hundi ya shilingi Bilioni 2 kutoka kwa Taasisi za Umma zilizotolewa ajili ya kusaidia maafa yaliyotokea Katesh.

"Walisema huyu mzee amekata moto, wengine waliweka picha yangu ya portrait na mshumaa unaowaka.,..Lakini Mh. Rais sisi viongozi ni binadamu na hii inaleta taharuki bila sababu....Tusitumie mitandao kueneza mabaya, Nina afya njema." Ameeleza.

Aidha ameeleza namna alivyompoteza dada yake mwaka 2021 baada ya baadhi ya mitandao ya kijamii kueleza kuwa kiongozi huyo amefariki.

 Dr. Mpango amewataka watanzania kuenzi misingi ilivyoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume kwa kujenga Taifa linalosimamia misingi ya haki, utu na amani.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...