Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance na Axieva, wamewafikishia wakazi wa Mbagala, jijini Dar es Salaam huduma ya Afya Bima ili kuwa na uhakika wa kupata tiba na kupunguza mzigo wa gharama za matibabu.

Baadhi ya wakazi wa Mbagala ambao wamejiunga na huduma hiyo wamesema imekuwa faraja kwao kupayta huduma hiyo kwa unafuu na kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wowote.

"Nimefurahi sana leo kupata huduma ya Afya Bima kwa kiasi kidogo cha fedha hii itanisaidia mimi pamoja na familia yangu kuipata matibabu wakati wowote bila ya kuwa na hofu" alisema Salma Michael, Mkazi wa Mbagala

"Ndoto yangu ya kuwa na Bima ya afya imetimia na mimi nimekuwa na uhakika wa matibabu wakati wowote, kwakweli nawashukuru sana Airtel Money kwa kutuletea bima hii nafuu kwa watanzania alieleza Bwana Pascal Bwire mkazi wa Mbagala

Meneja Huduma wa Airtel Money, Bi. Hellen Lyimo amesema, wao pamoja na Jubilee Insuarance wameanza kutoa bima ya gharama nafuu ya shilingi mia tatu ili kutoa fursa kwa kila mtanzania kunufaika na huduma za matibabu kupitia Afya Bima.

"Tumeweka njia rahisi kwa mtanzania na mtumiaji wa Airtel Money kupata huduma ya Afya Bima. Sisi pamoja na Jubilee insurance tunawahakikishia watanzania kupata huduma ya matibabu kwenye vituo zaidi ya 600 nchi nzima kwa gahama nafuu kabisa" alisisitiza Bi Hellen.

Vifurushi vinavyotolewa na Airtel Money sambamba na Jubilee Insurance ni Afya Poa, Afya Supa na Afya dhahabu.

Mkurugenzi wa Airtel Money, Bwana Charles Rugambwa (kulia), kikabidhi zawadi ya fulana Kwa baadhi ya wakazi wa mbagala, wakati wa tamasha lenye lengo la kuhamasisha watanzania kujiunga na huduma ya Afya Bima, inayotolewa na Airtel Money kwa kushirikiana na Kampuni za Jubilee Insurance na Axieva, wakati wa tamasha lenye lengo la kuhamasisha watanzania kujiunga na bima hiyo Ili kuweza kuokoa maisha yao na kupunguza mzigo wa gharama za matibabu. Hafla hiyo ilifanyika, Mbagala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana.

Meneja Huduma wa Airtel Money, Hellen Lyimo (kushoto), akitoa maelekezo ya jinsi ya kujisajili katika huduma ya Afya Bima, Inayotolewa na Airtel Money kwa ushirikiano na Kampuni za Jubilee Insurance na Axieva, wakati wa tamasha lenye lengo la kuhamasisha watanzania kujiunga na bima hiyo Ili kuweza kuokoa maisha yao na kupunguza mzigo wa gharama za matibabu. Hafla hiyo ilifanyika, Mbagala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Bwana Jackson Mmbando (kulia), akitoa maelekezo kwa mkazi wa mbagala jinsi ya kujisajili katika huduma ya Afya Bima na faida zake, wakati wa tamasha lenye lengo la kuhamasisha watanzania kujiunga na bima hiyo Ili kuweza kuokoa maisha yao na kupunguza mzigo wa gharama za matibabu. Hafla hiyo ilifanyika, Mbagala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Afya Bima inatolewa na Airtel Money kwa ushirikiano na Kampuni za Jubilee Insurance na Axieva.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya, akikonga nyoyo za maelefu ya wakazi wa mbagala na maeneo jirani waliojitokeza katika tamasha lenye lengo la kuhamasisha watanzania kujiunga na huduma ya Afya Bima inayotolewa na Airtel Money kwa ushirikiano na Kampuni za Jubilee Insurance na Axieva. Hafla hiyo ilifanyika, Mbagala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...