Maombi yakifanyika
Askofu wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni Dar es Salaam, Rose Mgetta akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha la SHILO lonalofanyika kila mwaka kanisani hapo.
Washiriki wakiburudika na kwaya
Askofu wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni Dar es Salaam, Rose Mgetta akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha la SHILO lonalofanyika kila mwaka kanisani hapo.
Washiriki wakiburudika na kwaya
Kwaya ikitumbuiza
Dk. Rose Rwakatare akizungumza kuhusu uzinduzi wa tamasha hilo siku ya Jumapili.Na Mwandishi Wetu
KANISA la Mlima wa Moto Mikocheni jijini Dar es Salaam, limezindua kongamano liitwalo SHILO kama sehemu ya kumuenzi mwanzilishi wa Kanisa hilo, Hayati Askofu Dk. Getrude Rwakatare.
Uzinduzi wa kongamano hilo la siku nane ambalo hufanyika kila mwisho wa mwaka ulifanyika siku ya Jumapili mara baada ya Ibada kanisani hapo na Askofu wa Kanisa hilo, Rose Mgetta.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kongamano hilo, Askofu Mgetta alisema kongamano hilo liliasisiwa na hayati Askofu Dk. Getrude Rwakatare na limekuwa likifanyika kila mwaka hata baada ya kifo chake.
“Maombi ya SHILO yalikuwa ni maono ya Askofu wetu mwanzilishi hayati Askofu Dk. Getrude Rwakatare na tumekuwa tukiyaendeleza mwaka hadi mwaka na makanisa yote ya Mlima wa Moto wamekuwa wakifanya maombi haya kila mwaka,” alisema
“SHILO ni majibu ya mwisho ya mtu ambaye amekata tamaa mfano ameshindwa kupata mtoto, ameshindwa kuolewa akija kwenye tamasha hili la siku nane la SHILO lazima jibu lake lipatikane,” alisema
Alisema wataendelea kuombea taifa liendelee kuwa na amani na kuondokana na majanga kama ukame na matatizo mbalimnbali yanayotokea kwenye jamii.
“Ili Kanisa liwe na amani lazima nchi iwe na amani kwa hiyo umekuwa wajibu wetu kuhakikisha tunaombea amani ya nchi mara kwa mara na tunamuombea Rais wetu Mungu aendelee kumpa afya njema aweze kuendelea kulikongoza vyema taifa letu,” alisema Askofu Rose
Naye Dk. Rose Rwakatare alisema kongamano la SHILO lilianza miaka 20 iliyopita katika Kanisa hilo lililoko Mikocheni B jijini Dar es Salaam.
“Hili kongamano tunakuwa nalo kila mwaka na lilianzishwa na marehemu Askofu Dk. Getrude Rwakatare sisi tunaliendeleza kumuenzi na tunaahidi kuendelea kumuenzi situ kwa kongamano hili bali kwa kazi zote alizokuwa akizifanya,” alisema
Alisema Askofu Dk. Getrude Rwakatare aliweka misingi mizuri ya Kanisa na ndiyo sababu limekuwa likiendelea kutoa huduma ya kiroho hata baada ya kuondoka kwake.
“Namshukuru Rose Mgeta kwa kusimamia maono haya na kuhakikisha kazi ya Mungu inaendelea na nashukuru kwa mzigo mkubwaa alionao Rose kuombea taifa hili ni watu wachache wanaojitoa kuombea taifa lakini Rose na kanisa wamesimama kuombea nchi dhidi ya majanga kama ukame,” alisema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...