Wafanyakazi wa Barrick wakipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu), Mh.Joyce Ndalichako.
Wafanyakazi wa Barrick wakifurahia tuzo ambazo kampuni imejishindia
---
Mgodi wa North Mara, unaomilikiwa kwa ubia kampuni ya Barrick Gold Corporation na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals Corporation, umeshinda tuzo kubwa ya Mwajiri Bora kwa mwaka huu inayotolewa na Chama Cha Waajiri nchini (ATE).


Mh. Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), alikuwa Mgeni Rasmi katika kutoa tuzo kwa washindi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.


Mbali na ushindi Mkubwa wa tuzo ya jumla, Migodi ya Barrick imeshinda Tuzo nyingine 5 ambazo ni Mshindi wa Jumla katika Sekta Binafsi (North Mara), Mshindi Bora katika utekelezaji wa sera ya Uwajibikaji kwa jamii (North Mara), Mshindi bora katika udhibiti wa Maafa (Bulyanhulu), Mshindi wa pili kutekeleza sera ya ushirikishaji wananchi katika mnyororo wa madini –Local content (North Mara) na mshindi wa jumla Taasisi kubwa zinazotoa ajira (North Mara).


North Mara, ni moja ya mgodi ambao umefanikiwa kuzalisha ajira nyingi kwa wananchi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja ambapo zaidi ya asilimia kubwa wanatoka katika vijiji vunavyozunguka mgodi huo.


Mgodi unaendelea na programu ya kutekeleza mradi kwa kilimo Biashara kwa lengo wa kupanua wigo kwa vijana wengi kujipatia kipato kupitia kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...