Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) imetangaza matokeo ya mitihani ya 98 iliyofanyika mwezi Novemba mwaka 2023 ya Bodi ambapo takwimu zinaonesha watahiniwa 6711 katika ngazi mbalimbali za masomo ya Bodi ufaulu ni asilimia 66.6
Akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema Ufaulu umepungua kutoka asilimia 67 mpaka 66.6 ambapo watahaniwa 527 hawakuweza kufanya mitihani kwa sababu mbalimbali, hivyo idadi ya watahaniwa 6711 sawa na asilimia 92.7 walifanya mitihani ambapo wanawake walikuwa 3636 sawa na asilimia 50.2 na wanaume 3602 sawa na asilimia 48.8
Pia Bodi hiyo imezindua mihutasari mipya pamoja na vitabu vya rejea ambapo Bodi ya NBAA hufanya mapitio ya mtaala yake pamoja na vitabu kila baada ya miaka mitano.
Maneno amesema Bodi ilianza mchakato wa kupitia mitaala yake pamoja na vitabu rejea kuanzia mwezi Agosti mwaka 2022 na zoezi hili lilianza kwa kufanya marekebisho ya Mtaala na baadae zoezi la kupitia vitabu rejea lilifanyika.
"Bodi inaendelea kuboresha mitaala ya kufundishia ili kuongeza idadi ya Wahasibu na Wakaguzi hapa nchini ili kuweza kuchangia katika maendeleo hasa kuhakikisha Hesabu tunazozitoa zinakuwa ni sahihi na zinaaminika." akisema Maneno
Pia CPA MAneno amesema Bodi itaendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali za elimu ili kuhakikisha maadili yanazingatiwa ili vijana waandaliwe tangu wakiwa vyuoni .
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno akizindua mitaala mipya ya masomo ya Bodi itakayoanza kutumika Januari mwaka 2024 na kuanza kufanyiwa Mitihani Novemba mwaka 2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno akionesha mitaala mipya ya masomo ya Bodi kwa waandishi wa Habari mara baada ya kuzindia mitaala hiyo iliyofanyika katika ofisi za Bodi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno akizundua vitabu vya rejea vitakavyoanza kutumika kuanzia mwaka 2024 wakati wa mkutano na waandishi wa habari waliofika ili kupata taarifa mbalimbali za Bodi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno akionesha vitabu rejea pamoja na Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo, Peter Lyimo(wa kwanza kushoto) na Mkufunzi CPA Rashid Mganwa(wa kwanza kulia) wakati wa kutangaza matokeo pamoja na kuzindua mitaala mipya wa masomo itakayoanza kutumika mwaka 2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kutangaza matokeo ya mitihani ya 98 ya Bodi, uzinduzi wa Mitaala mipya ya Bodi pamoja na Vitabu rejea pamoja na sheria ndogo za mafunzo ya Mitihani ya Wahasibi na Wakaguzi ya Mwaka 2023.
Mkutano ukiendelea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...