MARYAM Sombi ambaye ni mdogo wa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Rehema Sombi, amechaguliwa kwa kishindo kuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa kupitia Chipukizi.

Maryam (Sombi Jr) aliibuka mshindi katika uchaguzi mkuu wa tisa(9) wa Chipukizi uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma, jana, Desemba 20, 2023 ambapo alichaguliwa kwa kura 284 sawa na asilimia 90.7 zilizopigwa na wajumbe katika Mkutano huo.

Akizungumza baada ya kupewa dhamana hiyo, Sombi Jr aliahidi utumishi uliotukuka akisema katika kipindi chake cha uongozi atahakikisha anapigania maslahi ya watoto wa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wananchi na Tanzania kwa ujumla.

Katika mkutano huo Qailah Nurdin Bilal ambaye ni mtoto wa msanii wa muziki wa Bongofleva, Shetta, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa.

Qailah aliibuka kidedea baada ya kupata kura 303 kati ya 402 zilizopigwa na wajumbe hivyo kuwashinda wenzake aliokuwa akigombea nao katika uchaguzi huo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...