MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwajulisha wananchi katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es salaam kuwa ugawaji wa Vitambulisho kwa Umma unatarajia kuanza tarehe 12/12/2023 katika wilaya zote za mkoa huo.

Hivyo, wananchi wote waliosajiliwa na kupatiwa Namba za Utambulisho wa Taifa (NINs) mnaombwa kujitokeza na kuchukua vitambulisho katika ofisi za Serikali za mitaa, ndani ya siku kumi na nne (14) tangu kuanza kugawiwa kwa vitambulisho hivyo ndani eneo husika .

Mwananchi atakayeshindwa kuchukua Kitambulisho chake ndani ya muda uliopangwa katika eneo lake, atalazimika kukifuata Kitambulisho chake katika ofisi ya NIDA ya Wilaya anayoishi.

Usomapo au kusikia tangazo hili tafadhali mjulishe na mwingine.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano

MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA
Barabara ya Kilimani, S.L.P 12324, Dar es Salaam, Simu: +255734220962,
Barua pepe: info@nida.go.tz, Tovuti: www.nida.go.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...