Na Mwandishi Wetu

OFISA Utumishi wa Chama cha Walimu Tanzania( CWT) Taifa Neema Ezekia amesema maadhimsho ya siku ya walimu Duniani Kwa utaratibu wa Chama hicho yanafanyika kila baada ya miaka minne na mwaka huu yalikuwa yafanyike Novemba 4,2023 kwa ratiba iliyokuwa imepangwa.

Amesema maadhimisho ambayo yamefanyika katika ngazi za Wilaya ni kwa utaratibu ukizingatia siku hiyo ni siku ya walimu Duniani lakini kitaifa lazima yaadhimishwe kitaifa na yaratibiwe na ngazi ya juu ya Chama hicho.

Neema ameyasema hayo Desemban 8 ,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa kutolea ufafanuzi kuhusu malalamiko na shutuma zinazoletwa na baadhi ya walimu na wanachama waChama hicho.

Amesema kuwa wao kama Chama taifa hakiwezi kuwafunga walimu kufanya sherehe hizo kwenye ngazi za wilaya Kwa lengo la kusubiri sherehe ya ngazi ya kitaifa ila kile ambacho linakwenda kufanyika katika maadhimisho hayo basi hata hao walioadhimisha watakuwa ni miongoni mwa watakaoshiriki.

Akizungumzia Wilaya ambazo zilifanya maadhimisho hayo ya siku ya walimu Duniani ni kagera,kibiti ,Tanga Jiji na Kisarawe, hivyo msukumo mkubwa wa kufanya maadhimisho hayo ni kwasababu pia wanatukio moja kubwa la kutimiza miaka 30 ya kuzaliwa kwa CWT.

"Chama hiki kinatimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake, hivyo kupitia maamuzi yaliyotokana na vikao vya ndani ambapo yalikuwa nikufanya matukio hayo mawili kwa wakati mmoja na ndio maana wao wamekuja na maandalizi ya siku ya mwalimu Duniani lakini kikubwa ni maadhimisho ya miaka 30 ya Chama.

"Chama cha walimu sio chombo kidogo, ni kikubwa na jambo hili tunaliandaa katika ubora wake kwa maana ya kubeba taswira nzima ya Chama kama kilivyo na si vinginevyo " amesisitiza

Kuhusu taarifa za uwepo wa ufisadi ndani ya Chama hicho, amesema ni mambo ya ajabu kwani tukio lenyewe halijafanyika lakini wanashangaa kusikia baadhi ya watu wanazungumzia ufisadi kimsingi hakuna jambo linaloweza kufanyika pasipokuwa na maandalizi ila ieleweke jambo hilo ni kubwa na matarajio ya maadhimisho hayo ni kuwa na mgeni rasmi ambaye ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Dhana au taswira ya kuzungumzia ufisadi basi ipatikane baada ya shughuli nzima kukamilika kwasababu hapa siwezi kuzungumza ni katika maeneo gani ambao huo ufisadi unafanyika lakini tunalifanya kwa uratibu ambao uko wazi na mipango yote inaanzia kwenye vikao, "amesema

Amefafanua jambo hilo wanalokwenda kulifanya ni kubwa na wanakusudia kushiriki walimu takribani 40,000 na walimu wapo tayari kuhudhuria.Mwitikio ni mkubwa, lengo ni kuona hadhi ya siku ya mwalimu inafikiwa na wao kama Chama taifa ni kuhakikisha wanaratibu na kufanikisha kufanyika Kwa tukio hilo.

Hata hivyo Rais wa Chama cha walimu Tanzanaia CWT Leah Ulaya amewataka walimu nchini kupuuza taarifa za upotoshaji zinazoendelea kwani maadhimisho hayo yameratibiwa na vikao halali vya Chama cha walimu Tanzanaia.

"Kwahiyo Kila mmoja anafahamu kwenye vikao hivyo tuna uwakilishi wa kutosha katika maamuzi Kila mkoa tumepta wajumbe takribani saba na hao Saba wanaporudi mikoani kwao wanakwenda mpaka wilayani kutoa taarifa.

"Bahati nzuri maadhimisho haya yamekubaliwa na kuratibiwa Baraza Kuu la Taifa ambapo chombo hicho ndio chombo pekee kinaratibu na kupanga bajeti za Chama."

Ameongeza katika maadhimisho hayo wanatarajia mgeni rasmi kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambapo wao kama Chama wanapanga jambo la kuwasilisha mbele ya mkuu wa nchi.

Amesema anaamini uwepo wa Rais Dk. Samia utatoa nafasi kwa Rais kuzungumza au kuelekeza mambo mbalimbali ya kielimu na hata kwa jamii ya watanzania wote.

Ofisa Utumishi wa Chama Cha Walimu Tanzania(CWT) Taifa Neema Ezekia akizungumza mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya kuelekea kwenye maadhimisho ya Siku ya Walimu ambayo inakwenda Sambamba na kumbukizi ya kutimiza miaka 30 ya Chama hizo .Sherehe hizo zitafanyika jijini Mwanza
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...