Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii wa Japan Konosuke Kokuba anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania Januari mwaka 2024.

Katika ziara hiyo, Kokuba ataongozana na ujumbe wa watu 40 kutoka kampuni binafsi zinazojihusisha na masuala ya miundombinu na baadhi ya watumishi wa Wizara yake.

Ziara hiyo imelenga kujadili fursa mbalimbali zinazotokana na ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika maendeleo ya miundombinu.

Hayo yalijulikana katika kikao cha pamoja cha maandalizi ya ziara hiyo kilichoshirikisha viongozi wa Wizara ya Uchukuzi na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa pamoja na Menejimenti yake kilichofanyika jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara.

Kwa upande wa Japan, ujumbe wake uliongozwa na Bwana Yoshihiro Kakishita kutoka Sekretarieti ya Wizara ya Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii ya Japan.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA Plasduce Mbosaa ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Japan kuja kuwekeza kwa upande wa miundombinu ya Bandari nchini.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Profesa. Godius Kahyarara akimpa zawadi mgeni wake Yoshihiro Kakishita kutoka Sekretarieti ya Wizara ya Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii ya Japan wakati wa kikao hicho ambacho kiliongozwa na Katibu Mkuu huyo. Anayeonekana kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA Plasduce Mbossa

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...