Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria uzinduzi wa Mchakato wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Rais Samia alifanya uzinduzi huo wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 09 Desemba, 2023.



Viongozi, pamoja na wageni mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na uzinduzi wa Mchakato wa ukusanyaji maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 9 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Gilead Teri wakati akielezea majukumu ya Kituo wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Lawrence Mafuru pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati ya Uongozi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali kabla ya kuzindua Mchakato wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Rais Samia alifanya uzinduzi huo wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameainisha changamoto zinazopaswa kupewa kipaumbele ikiwemo kufungamanisha ukuaji wa uchumi na sekta za uzalishaji.


Rais Samia amesema hayo kwenye maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara sanjari na Mkutano wa kwanza wa uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.


Aidha Rais Samia ametaka sekta mbalimbali za uzalishaji ziimarishwe zaidi ikiwemo kilimo ambayo inakua kwa asilimia 4 tu kwa sasa tofauti na inavyotakiwa.


Pia amesisitiza kuimarishwa kwa ushiriki wa sekta binafsi ndani na nje ya nchi ili kufanya wenyeji kuwa na utayari wa kupokea na kushirikiana na wageni wanaokuja kuwekeza na kufanya biashara nchini.


Rais Samia amesema dira hiyo mpya itatakiwa kuzingatia kigezo cha kuongeza pato la kila mwananchi kufikia dola za Kimarekani 3,000 kwa mwaka ambacho hakikufikiwa katika dira ya mwaka 2000-2025.


Amesema kushindwa huko kulisababishwa na ukuaji wa uchumi kutojielekeza kwenye sekta zinazogusa maisha ya watu wengi, hivyo umasikini vijijini haujapungua kwa kasi iliyotarajiwa.


Kuhusu suala la Maadili ya Taifa (ethos), Rais Samia amesema ni muhimu taifa kuwa na watu mahiri, makini na waadilifu ili kupata jamii inayochukia rushwa kila mahali, inayojituma na kufanya kazi bila kusukumwa na inayopinga na kulaani ukwepaji kodi.


Vile vile, Rais Samia ametoa wito kwa Watanzania wote ndani na nje ya nchi (Diaspora) kushiriki kutoa maoni katika kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo kupitia njia za kisasa zitakazoainishwa na Tume ya Mipango.



Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...