Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda mara baada ya yeye na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, walipowasili kukagua shule za Msingi ya Maji Matitu iliyoko Mbagala jijini Dar es salaam leo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, wakikagua moja ya madarasa ya shule ya Msingi ya Maji Matitu iliyoko Mbagala jijini Dar es salaam leo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimtambulisha Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, walipokuwa katika shule ya Msingi ya Maji Matitu iliyoko Mbagala jijini Dar es salaam leo. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimtambulisha Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, wakifurahi na wanafunzi walipotembelea  shule ya Msingi ya Maji Matitu iliyoko Mbagala jijini Dar es salaam leo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, wakitembelea madarasa ya  Shule ya Msingi ya Mikongeni iliyoko Gongo la Mboto jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, wakitembelea Shule ya Msingi ya Mikongeni iliyoko Gongo la Mboto jijini Dar es salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Deo Ndejembi


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimtambulisha Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, wa walimu na wanafunzi wa  Shule ya Msingi ya Mikongeni iliyoko Gongo la Mboto jijini Dar es salaam.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, leo wametembelea na kukagua shule za Msingi ya Maji Matitu iliyoko Mbagala na Mikongeni iliyoko Gongo la Mboto jijini Dar es salaam. 

 

Ziara hiyo, ambayo Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Juma Kipanga na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Deo Ndejembi pia walikuwepo, imefanyika siku tatu kabla ya mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi wa GPE utakaofanyika Zanzibar kuanzia mapema wiki ijayo.

 

Madhumuni ya ziara hiyo ilikuwa ni kukagua na kujionea shule ambazo Shirika hilo limetoa ufadhili.

 

Katika shule ya Maji Matitu shirika hilo limefadhili ujenzi wa  madarasa nane na matundu 20 ya vyoo,  wakati  katika shule ya Mikongeni imechangia ujenzi wa madarasa mawili na matundu sita ya vyoo.

 

Akiongea baada ya ziara hiyo, Dkt. Kikwete ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea kushirikiana na GPE katika kuboresha sekta ya elimu hasa hasa kwa wasichana na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi na mikakati ya kuiendeleza sekta hiyo.

 

Dkt. Kikwete, ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuongoza GPE, amesema shirika hilo hadi sasa limeishaipatia Tanzania jumla ya  Dola za Kimarekani Milioni 332 (takriban shilingi 834,980,332,000.00) ili kusaidia sekta ya elimu bara na visiwani.

 

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE Bibi Frigenti ametoa wito kwa wadau wa maendeleo kuendelea kusaidia juhudi za kuendeleza sekta ya Elimu hassan kaika nchi zenye uhitaji, akisisitiza kwamba changamoto nyingi za kimaisha zinaweza kuepukika endapo wananchi watapatiwa elimu bora.

 

Bi. Frigenti ameelezwa kuruidhishwa kwake na matumizi ya Fedha ambayo GPE imekuwa ikitoa kwa Tanzania na kusema kuahidi kuendeleza uhusiano mzuri uliopo na uliodumu kwa miaka 10 sas.

 

Bi Fringeti ameisifia serikali  kwa kuendelea na juhudi zake za kuendeleza elimu kwa kujenga miundo mbinu bora na kuhakikisha kila mtoto anapatiwa elimu.

 

Jana November 3, 2023 GPE imetiliana saini na Serikali ya makubaliano ya kutoa dola za Kimarekani milioni 85 (takriban shilingi 213, 775, 085, 000.0)    kwa ajili ya kusaidia mafunzo ya  walimu nchini.

 

Aidha, Dkt. Kikwete, akiwa mwenyekiti wa GPE ataongoza vikao vya Bodi vya Shirika hilo huko Zanzibar kuanzia tarehe 4 hadi 6 Disemba, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa Shirika hilo la kimataifa kufanya vikao vyake vya bodi barani Afrika..

 

GPE iliyoanzishwa mwaka wa 2002, ni Shirika linalosimamiwa na Benki ya Dunia, linalofadhili  maendeleo ya  elimu ya msingi na utendaji wa sera za nchi zinazoendelea. 

 

Majukumu ya GPE ni pamoja na  kusaidia serikali za nchi zinazoendelea kufanya mabadiliko ya kimfumo na kuoanisha rasilimali na ufadhili ili kutoa elimu bora kwa watoto Wote, kuinua viwango vya kujifunza na kukabiliana na changamoto mpya.

u nchini.

 

Aidha, Dkt. Kikwete, akiwa mwenyekiti wa GPE ataongoza vikao vya Bodi vya Shirika hilo huko Zanzibar kuanzia tarehe 4 hadi 6 Disemba, na tayari wajumbe wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali duniani wameanza kuwasili nchini.

  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...