Na Oscar Assenga, TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amewaasa wananchi wa mkoa huo kucha tabia ya kuwanyanyapaa na kuwabagua watu wanaoishi na Ugonjwa wa Ukimwi kwenye ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.

Wito huo uliotolewa katika Hotuba yake iliyosoma kwa niaba yake Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Tangamano.

Alisema kwamba jamii inapaaswa kuacha kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vinachangia maambukizi mapya ya VVU.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba lazima Watumishi Idara ya Afya waendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa afuasi mzuri wa dawa na kufuatilia kiwango cha VVU kwa wanaopokea huduma wanaowahudumia.

Aidha pia Mkuu huyo wa Mkoa aliitaka Idara ya Afya na Maendeleo ya Jamii kuendelea kuwashauri wananchi ambao hawajui afya zao umuhimu wa kupima afya .

“Lakini pia shirikianeni na wadau waliopo mkoani kufanya kampeni maalumu kwenye maeneo yenye viashiria vya uhatarishi wa maambukzi ya VVU sambamba na kuimarisha utendaji wa kamati shirikishi za Ukimwi katika ngazi za vijii,mitaa,kata na wilaya ili ziweze kuratibu vyema huduma za ukimwi kwenye maeneo yetu”Alisema

Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuendelea kujali makundi yote yenye uhitaji maalumu nchini ikiwemo wale walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.

“Tumeona kwenye mabanda tuliotembelea jinsi walivyosaidiwa na kuweza kujikita kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi ili waweze kujikimu mahitaji yao ya kila siku na jinsi huduma zinavyotolewa za kuondoa unyanyapaa katika Jamii”Alisema

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya Ukimwi Kitaifa yamefanyika Mkoani Morogoro yaliobeba kauli Mbiu ya mwaka huu Jamii iongoze kutokomeza Ukimwi na hiyo inahimiza umuhimu wa kutoa nafasi kwa jamii kushika hatamu katika jitihada za kutokomeza ukimwi.

Hivyo ni Rai yangu kwa Asasi za Kiraia ambazo zinashirikisha makundi mbalimbali ya kijamii hasa zenye hatari ya kupata maambukizi ya VVU kuwa mstari wa mbele kwenye kupambana na kutekeleza afua mbalimbali za ukimwi kwenye mkoa huo.

Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Tanga Dkt Suleiman Msangi alisema kwamba maambukizi ya Ukimwi bado ni makubwa katika mkoa huo hivyo wanahitaji wadau wote waongeze mikakati ya kukabiliana na hali hiyo ikiwemo utoaji wa elimu kwenye majukwaa mbalimbali, muhadhara, kiasiasa na dini.

Alisema mkoa wa Tanga wanaendelea na mapambano mbalimbali ya kuhakikisha wanatokomeza maambukizi ya VVU ikiwemo upimaji wa VVU ambao unaendelea kwa wananchi kwenye vituo vya Serikali na Binafsi.

Dkt Msangi alisema kwamba mkoa huo umepata mdau anayefuatilia ndugu mwenye kifua kikuu anayegundulika na ukimwi na dawa za kupunguza makali ya VVU na Ukimwi zinaendelea kutolewa bila malipo kwa mtu yeyote anayegundulika na kuishi navyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...