Ubalozi wa Marekani unafuraha ya kutangaza ushirikiano na WiLDAF katika harakati za kutokomeza ukeketaji. Kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Afrika (ARDF), Ubalozi unafadhili mradi wa miezi 18 wa WiLDAF uitwao ‘Kutokomeza Ukeketaji mkoani Mara-Jamii Imara’ utakaotekelezwa mkoani Mara. Mradi unalenga kuchangia katika kuongeza kasi ya kutokomeza ukeketaji nchini Tanzania kama ilivyoainishwa katika Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Ukeketaji. Mradi huu wa ‘Jamii Imara’ utatekelezwa katika wilaya tatu za Mara: Tarime, Butiama, na Serengeti.

Lengo la mradi wa ‘Jamii Imara’ ni kukuza maadili ya kijamii na kijinsia katika kutokomeza ukeketaji. Mradi utafanyakazi na vikundi vya wanawake na wasichana ili kuwawezesha kupata uelewa juu ya haki zao na masuala ya kijinsia. Kwa wanawake na wasichana wasio mashuleni, mradi unajumuisha kipengele cha uwezeshaji kiuchumi ili kutoa vyanzo mbadala vya mapato, kujenga uwezo wa kifedha na kupunguza uwezekano wa ukeketaji na aina nyingine za ukatili wa kijinsia.

Pia, mradi wa Jamii Imara utafanya kazi na vijana wa kiume, viongozi wa kidini na kimila ili kuwa mashujaa wa mabadiliko na kuongoza mipango ya mabadiliko ya kijamii katika ngazi za chini. Katika ngazi ya kitaasisi, Jamii Imara itasaidia ujenzi wa mitandao imara ya asasi za kiraia na serikali kwaajili ya kujifunza kwa pamoja, kubadilishana uzoefu, kushirikiana na kuimarisha hatua za pamoja za kukomesha ukeketaji wa aina zote, ikiwa ni pamoja na mila zinazovuka mipaka.

Katika maadhimisho ya mwaka huu ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, mradi wa ‘Jamii Imara’ ni dhamira ya Serikali ya Marekani ya kuendelea kuwekeza na kusaidia asasi za kiraia na Serikali ya Tanzania katika mipango inayolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. 


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...