SERIKALI ya awamu ya nane chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi, ndani ya miaka mitatu ya uongozi wake ametenga kiasi cha shilingi bilioni 50 kwa ajili ya mikopo ya vikundi vya Wajasiriamali nchini.

Kauli hiyo ametolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis wakati akizungumza katika hafla ya kumpongeza Rais wa Zanzibar Dk.Hussein iliyoandaliwa na Wadi ya Wara Jimbo la Wawi uko ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Pemba.

Amesema lengo la mikopo hiyo yenye masharti nafuu ni kuhakikisha wajasiriamali wanapata fedha za uhakika katika kutekeleza miradi yao.

Alieleza kuwa Dk.Mwinyi, ameendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi zote alizotoa katika uchaguzi mkuu wa dola uliopita wa mwaka 2020 ili kuhakikisha wananchi wote wa mijini na vijijini wananufaika.

“Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ametenga fedha hizo zaidi ya bilioni 50 hivyo wananchi endeleeni kuunda vikundi mpate mikipo hiyo na kunufaika bila kujali tofauti za kisiasa.”,alisema Mbeto.

Katika maelezo yake Mbeto, aliwambia wanachama hao wa CCM kuwa Serikali hiyo inayoongozwa na Dk.Mwinyi imefanya mambo mengi ya maendeleo na kuimarisha ustawi wa kijamii zikiwemo kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma pamoja na pencheni ya wazee wenye umri wa miaka 70 hadi kufikia kiasi cha shilingi 50,000/= kwa kila mwezi. Pamoja na hayo alieleza kwamba katika suala la utekelezaji wa Ilani Dk.Mwinyi tayari kuna maeneo amevuka malengo kwa zaidi ya asilimia 100, zikiwemo sekta za elimu na afya na uwezeshaji wananchi kiuchumi.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...