WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kaskazini Pemba, wameshauriwa kujitokeza na kutoa ushirikiano katika zoezi la uandikishaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura ili kupata wanachama wenye sifa za kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis wakati akizungumza na Wanachama na Wananchi kwa ujumla mara baada ya kutembelea Vituo vya uandikishaji wa Daftari hilo Kisiwani Pemba.
Alisema kila mwanachama anatakiwa kutoa taarifa sahihi pamoja na kuhakikisha anafanya marekebisho ya kina katika taarifa zake kwa lengo la kupata uhalali wa kisheria wa kuwa miongoni mwa wananchi wenye sifa za kuingia katika daftari la kudumu la wapiga kura.
“Tumepita katika Vituo mbalimbali vya uandikishaji wa zoezi hilo na kubaini kuwa linaendelea vizuri na wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi hali inayotoa taswira ya uwepo wa Amani na utulivu.
Natumia nafasi hii kuwaomba sana wanachama,viongozi na watendaji wetu kuanzia ngazi za mashina hadi Taifa kulipa kipaumbele zoezi hili kwa kuhamasisha wanachama wetu na wananchi wote wenye sifa kwenda kujiandikisha na kufanya uhakiki wa taarifa zao katika vituo hivyo.”, alisema Mbeto.
Pamoja na hayo alisema kwamba kwa upande wa CCM zoezi hilo ni muhimu sana kwani ndio sehemu pekee ya kujitathimini kisiasa kwa nia ya kujipanga katika kupatikana kwa ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Mbeto,alifafanua kwamba kutokana na muamko na uelewa mpana wa Wananchi wa Kisiwa cha Pemba anatarajia zoezi hilo litaendelea kufanyika kwa Amani na utulivu huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kukamilisha wajibu wao wa kisheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...