Na.Elimu ya Afya kwa Umma.
Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kinga Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani imefanya kikao cha wadau wa Afya Moja katika kukabiliana na magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kuanzia tarehe 13 Disemba Hadi tarehe 15 Disemba 2023 Mjini Morogoro.
Kikao kimekutanisha Wadau kutoka Wizara ya Afya na Wizara mtambuka na Taasisi kama vile (Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ofisi ya Waziri Mkuu, Maji, Kilimo, Mifugo, Elimu) Taasisi za Utafiti, Vyuo Vikuu, na Wadau wa Maendeleo
Kikao kililenga kufanya uchambuzi wa awali (situation analysis) wa mbinu ya Afya Moja katika kukabiliana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele hasa yale yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
Akifungua Kikao hicho Dkt. Tumaini Haonga ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga amesema
"Tanzania inajivunia kuanzishwa kwa Kurugenzi Maalum ya Uratibu wa Afya Moja ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, yenye lengo la kuoanisha afua katika Wizara zote ili kudhibiti Magonjwa yanayohitaji ushirikishwaji wa Sekta mbalimbali.
Zaidi ya hayo, amesema Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele (NTDCP), ulianzishwa mwaka 2009 chini ya Wizara ya Afya ili kuweza kuratibu Magonjwa haya.
Hata hivyo, licha ya juhudi hizi zilizoratibiwa, bado Magonjwa ya NTDs hasa yanayoambukizwa kutoka wanyama kwenda kwa binadamu yanaendelea kupokea uangalizi duni kutoka kwa mifumo ya huduma za afya, taasisi za utafiti, Elimu na watunga Sera"amesema.
Home
AFYA
WIZARA YA AFYA ,WADAU WA AFYA MOJA WAJADILI KUKABILI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...