Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amewataka wauni wa Dini ya Kiislamu na  Wazanzibar kwa ujumla kuhakikisha wanasimamia maadili hasa kwa vijana ili kupata  vizazi zilivyo bora hapa nchini.


 Alhajj Hemed ameyasema hayo alipokuwa akiwasalimia waumini wa Masjid SHURAA  MUEMBE MAKUMBI MASUMBANI  mara baada ya kumaliza  Ibada ya Sala ya Ijumaa.

 Amesema kuwa kuwepo kwa  maadili mema kwa vijana kutapelekea  kuondosha kabisa vitendo vya uzalilishaji na matumizi ya madawa ya kulevya ambavyo vinaathiri vizazi vyetu na  kuiharibia sifa nchi yetu ya Zanzibar.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ni wajibu wa kila Mzanzibari kupiga vita suala la udhalilishaji hasa kwa wanawake na watoto ambao ndio wahanga wakubwa wanaoathirika na vitendo hivyo viovu sambamba na kuhakikisha wanarejesha maadili ya kizanzibari ambayo ni urithi kutoka kwa wazee wetu.

 Alhajj Hemed amewataka waumini na  Wazanzibari wote kuhakikisha wanaitumia Misikiti kwa kuzungumzia masuala ya uzalilishaji na kuomba dua maalumu ili Mwenyezi Mungu aliondoshe janga hili katika Visiwa vyetu na Tanzania kwa ujumla.

 Akizunguzia suala la madawa ya kulevya  Alhajj Hemed amewataka wananchi wa Zanzibar  kushirikiana na Serikali katika kupiga vita madawa vya kulevya amabayo yanaendelea kuimaliza jamii ya wazanzibari hasa vijana.

Amesema Zanzibar ni nchi ya visiwa na ina Bandari kavu nyingi ambazo zinatumika kwa shuhuli mbali mbali hivyo ni lazima kuwepo na ushirikiano wa hali ya juu baina ya Serikali na Wananchi katika kuwafichua  wauzaji, wasambazaji na watumiaji wa madawa ya kuleva ili kupata vijana watakaoweza kulitumikia Taifa kwa uzalendo na weeledi wa hali ya juu.

 Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi itahakikisha inapambana katika kupiga vita uzalilishaji na madawa ya kulevya kwani Zanzibar bila ya majanga hayo inawezekana.

 Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Maalim SALUM ALI  amewataka waumini wa dini ya Kiislam kuwa na utamaduni wa kutoa sadaka kwa kile ambacho wamedirikiwa wa Mwenyezi Mungu ili kupata ujira hapa duniani na kesho akhera.


 Amesema kuwa uislamu kupitia kitabu kitakatifu cha Quran umeamrisha waumini kutoa sadaka, kuwahurumia mayatima, kuwasaidia wajane na wasiojiweza ili kuwasaidia waweze kujikimu na kupunguza wimbi la matendo maovu yanayochafua taswira ya Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...