Na Pamela Mollel,Arusha
Viongozi wa Mila wa jamii ya wafugaji kutoka tarafa tatu za wilaya ya longido Mkoani Arusha wameanza kuchukua hatua za kuyatambua na kuyalinda maeneo yote yaliotengwa kwaajili ya nyanda za malisho ya mifugo
Hatua hiyo imekuja kipindi ambacho mvua zinazoendelea kunyesha hali itakayosaidia kukabiliana na ukosefu wa malisho wakati wa kiangazi
Wakizungumza wakati wilipokutana Viongozi wa mila kujadili njia bora za kusimamia nyanda hizo na kushughulikia changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi
Kiongozi wa mila Saron Kayongo kutoka longodo anasema wanaamini majadililiano hayo na wadau wahifadhi itasadia kwa kiwango kikubwa kulinda maeneo yaliyohifadhiwa ya nyanda za malisho
Afisa uhifadhi jamii na mazingira kutoka shirika la watu na wanyamapori TPW linalowajengea wafugaji uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi bwana Kirerenjo Medukenya anasema sababu za kukutanisha kundi hilo kwaajili ya kutoe elimu na mafunzo kwa Viongozi hao wa mila ili kutambua faidia ya kuhifadhi nyanda za malisho
Kwa upande wake Afisa mazingira kutoka ofisi ya Rais Tamisemi Theodori Mlokosi anasema a kikao hicho kina manufaa makubwa kwa jamii kwani kitasaidia kuondosha migogoro ya wakulima na wafugaji
Wilaya ya longido ambayo aslilima kubwa ya wakazi wake ni wafugaji imekua ikikabiliwa na ukame wa muda mrefu unaoathiri malisho na wakati mwingine baadhi kulazimika kuhama makazi yao kwa ajili ya kunusuru mifugo yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...