Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mhe Juma Chikoka amepokea vitambulisho vya Taifa (NIDA) 85,000 na Kuwakabidhi kwa watendaji wa Kata 26 za Wilaya ya Rorya amabao na wao wataenda kusimamia zoezi la ugawaji kwa vijijini vyote 87 vya Rorya.
Lengo ni kuhakikisha Vitambulisho vinawafikia wananchi walipo hususani vijijini ambao wengi walikua na namba tu lakini sasa watakua na vitambulisho.
''Shukran za Kipekee kwa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha fedha za kupatikana kwa vitambulisho hivi'', amesema Chikoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...