Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) kutoka Vodacom Tanzania akifurahi pamoja na mmojawapo wa akina mama waliopatiwa bima ya bure kwa mwaka mzima katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou-Toure jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni yake inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, kampuni hii imekabidhi kadi za bima kwa akina mama 100 na watoto 100 hospitalini hapo ikiwa ni zawadi ya upendo kutoka kwa kampuni hiyo katika msimu huu wa sikukuu.
Mshindi wa pesa taslimu shilingi milioni 10 kupitia kampeni ya Vodacom Tanzania PLC inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, Bw. Simon Bundala (wa pili kulia) akiwa ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa na Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) pamoja na msanii wa Bongo Flava, Dogo Janja (wa kwanza kushoto) na Straton Mchau, Meneja Mauzo Mwandamizi Kanda ya Ziwa (wa pili kushoto) katika viwanja vya Posta jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hii wateja wanayo fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...