Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) hii leo imewapokea wafanyakazi wake na wadau mbalimbali wa utalii wakiwemo waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro ambao wameshuka kutoka kwenye kilele cha Mlima mrefu zaidi duniani (uliosimama peke yake), Mlima Kilimanjaro. Wafanyakazi hao walipanda mlima huo kwa lengo la kufikisha mashine ya kufanyia miamala (POS Machine) ya benki hiyo kwenye kilele cha mlima huo.

Hatua hiyo mbali na kusogeza huduma za benki ya NBC wateja wake wanaotembelea mlima huo pia ililenga kudhihirisha umahiri wa teknolojia ya benki ya NBC katika utoaji wa huduma zake kwa wateja hususani kupitia mashine hiyo ya kisasa.

Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao waliopanda mlima huo Disemba 16 wakiongozwa na Bw Dickson Busagaga ambae ni mdau wa habari mkoani Kilimanjaro ilifanyika kwenye eneo la geti la lango la Marangu ikiongozwa na Afisa Uhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Gladys Ngu’umbi sambamba na Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru, wafanyakazi wa benki ya NBC, baadhi ya wadau wa utalii pamoja na wateja wa benki hiyo mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Bi Ngu’umbi pamoja na kuwapongeza wafanyakazi na wadau hao kwa kufanikisha zoezi hilo, pia aliipongeza benki hiyo kwa kuutumia mlima huo kama kigezo cha kuthibitisha ubora na ufanisi wa mashine hiyo ya miamala pamoja na kusogeza huduma hiyo kwenye kivutio hicho cha kimataifa, hatua aliyoitaja kuwa itasaidia sana kurahisisha huduma za malipo mbambali yanayofanywa na wageni mbalimbali wanaotembelea hifadhi hiyo.

‘’Kwetu sisi kama wadau wa utalii ujio wa huduma hii ni mkombozi dhidi ya changamoto ya huduma ya malipo iliyokuwa ikiwakabili wadau mbalimbali hususani wasindikiza wageni. Baadhi yao walikuwa wanalazimika kuwafuata watalii hadi nje ya hifadhi huko ili tu kufuata malipo yao.’’

“Kupitia mashine hii sasa malipo yao yanaweza kufanyika huko huko kwenye kilele wakiwa wanajipongeza’’ alibainisha Bi Ngu’umbi kauli ambayo iliungwa mkono na Bw Hillary Kombe na Godlisten Mkonyi wanaotoa huduma za kusindikiza wageni kwenye mlima huo.

Kwa upande wake Bw Ndunguru alisema hatua hiyo sio tu njia ya kuangazia sifa na kutangaza mashine hiyo ya POS bali pia kuunga mkono jitihada za serikali katika kukuza utalii wa ndani na nje kwa kuutangaza mlima huo mrefu zaidi barani Afrika na Duniani kwa ujumla.

“Tunatabasamu siyo tu kama washindi ila kwa kumshukuru Mungu kwa kutupa usalama na afya kufanikisha zoezi la kufikisha tabasamu hadi kilele cha mlima Kilimanjaro ambapo POS za NBC sio tu zimefika kilele cha mlima Kilimanjaro, bali pia zimewaka na kufanya miamala.’’

“Tunajivunia kuwa waanzilishi wa uzinduzi wa kwanza wa mashine ya POS katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. POS zetu zimeweza kufanya miamala katika vituo vyote, Mandara, Horombo, Kibo, Gilmans Point, Stella na hadi Uhuru Kileleni. Hii ni kuwahakikishia wateja wetu kuwa Mashine za POS ni imara, za uhakika na zinafanya kazi wakati wowote, kwenye mazingira yoyote na hali ya hewa yoyote. “ alibainisha Ndunguru.

Zaidi alisisitiza kuwa : ‘Sababu ya uzinduzi wa mshine hii katika kilele cha Mlima wa Kilimanjaro pia inatokana na sifa kuu tano zinazoendana na alama na maana ya vituo tunavyokutana navyo katika kupanda mlima huu. Tunaamini kila kituo kimeoana na sifa za mashine zetu za POS za NBC ambazo ni Urahisi, Haraka au Kasi, Teknolojia ya hali ya juu, Mahiri (Smart) na Uhuru wa malipo. Hatua hii inafuingua rasmi pazia la kuruhusu malipo kwa chaguzi mbalimbali za kidigitali kama vile Apple Pay , Google Pay, Amazon Pay, Samsung Pay na kadi yoyote ya benki. au hata kwa kutumia saa ya kidigitali''. alitaja.

Jitihada hizo ni muendelezo wa kampeni yetu mpya ya "Tabasamu Tukupe Mashavu," ya benki hiyo inayolenga kutoa fursa kwa wateja kufurahia pamoja na wapendwa wao wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki katika Sikukuu za mwisho wa mwaka kupitia miamala iliyorahishwa kupitia benki ya NBC.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi waliopanda mlima huo Bi Florence Ng’wavi ambae ni Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Barabara ya Meru alisema mafanikio hayo yanawasilisha adhima ya pamoja ya wafanyakazi wa benki hiyo katika kuthibitisha na kutetea ubora wa huduma wanazozitoa kwa wateja wa benki hiyo.

“Pamoja na changamoto mbalimbali tulizokumbana nazo wakati wa zoezi hili, bado tuliona ni rahisi zaidi kwasababu kila kituo tulichokuwa tunapanda kilikuwa kinathibitisha sifa moja wapo muhimu kwenye mashine hii. Kwa kuamini hivyo ikawa ni rahisi kwetu kwa kuwa tuliongozwa na dhamira ya kuthibitisha kile tunachokiamini yaani ufanisi na ubora wa huduma hii muhimu,’’ alisema Bi Florence.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru (wa saba kushoto)sambamba na Afisa Uhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Gladys Ngu’umbi (wa saba kushoto)   wakionesha  mashine ya kufanyia miamala (POS Machine) ya benki hiyo muda mfupi baada ya kurejea kutoka safari ya kihistoria ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kufikisha mashine ya hiyo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro ili kusogeza huduma za benki hiyo kwa wateja wake wanaotembelea mlima huo. Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao  hao imefanyika hii leo kwenye eneo la geti la lango la Marangu, Mkoani Kilimanjaro.

Maafisa waandamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), akiwemo Afisa Uhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Gladys Ngu’umbi (wa pili kushoto) wakiwapongeza baadhi ya baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na wadau wa utalii mkoani humo wakiwemo waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurejea kutoka safari ya kihistoria ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kufikisha mashine ya kufanyia miamala (POS Machine) ya benki hiyo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro ili kusogeza huduma za benki hiyo kwa wateja wake wanaotembelea mlima huo.Anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru (wan ne kulia). Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao imefanyika hii leo kwenye eneo la geti la lango la Marangu, Mkoani Kilimanjaro.

Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru (Kushoto) akimpongeza baadhi ya baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na wadau wa utalii mkoani humo wakiwemo waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurejea kutoka safari ya kihistoria ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kufikisha mashine ya kufanyia miamala (POS Machine) ya benki hiyo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro ili kusogeza huduma za benki hiyo kwa wateja wake wanaotembelea mlima huo. Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao imefanyika hii leo kwenye eneo la geti la lango la Marangu, Mkoani Kilimanjaro.


Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao waliopanda mlima huo Disemba 16 wakiongozwa na Bw Dickson Busagaga (wa tatu kushoto) ambae ni mdau wa habari mkoani Kilimanjaro ilifanyika kwenye eneo la geti la lango la Marangu ikiongozwa na Afisa Uhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Gladys Ngu’umbi (wanne kushoto)  sambamba na Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru (wa tano kushoto) wafanyakazi wa benki ya NBC, baadhi ya wadau wa utalii pamoja na wateja wa benki hiyo mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC mkoani Kilimanjaro na Arusha wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru (kushoto)  wakiwapongeza wenzao muda mfupi baada ya kurejea kutoka safari ya kihistoria ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kufikisha mashine ya kufanyia miamala (POS Machine)  ya benki hiyo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro ili kusogeza huduma za benki hiyo kwa wateja wake wanaotembelea mlima huo. Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao imefanyika hii leo kwenye eneo la geti la lango la Marangu, Mkoani Kilimanjaro.

Afisa Uhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Gladys Ngu’umbi (katikati)   akionesha  mashine ya kufanyia miamala (POS Machine) ya benki ya NBC ikiwa ni ishara ya kutambulisha huduma hiyo kwenye hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na maeneo mengine nchini wakati wa hafla ya kuwapokea wafanyakazi wa benki hiyo pamoja wadau wa utalii mkoani Kilimanjaro wakiwemo Waandishi wa habari waliorejea kutoka safari ya kihistoria ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kufikisha mashine ya hiyo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro ili kusogeza huduma za benki hiyo kwa wateja wake wanaotembelea mlima huo. Wanaoshuhusia ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru (kushoto)  na Ofisa Mwandamizi wa benki hiyo Bi Dogo Ramadhani (Kulia).Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao  hao imefanyika hii leo kwenye eneo la geti la lango la Marangu, Mkoani Kilimanjaro.
Hafla hiyo ilihusisha utoaji wa vyeti wa utambuzi na pongezi kwa wafanyakazi wa benki hiyo pamoja wadau wa utalii mkoani Kilimanjaro wakiwemo Waandishi wa habari waliorejea kutoka safari ya kihistoria ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kufikisha mashine ya hiyo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro ili kusogeza huduma za benki hiyo kwa wateja wake wanaotembelea mlima huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...