NA MWAMNDISHI – DODOMA
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amepokea Fedha Taslimu kiasi cha Shilingi Milioni Mbili na elfu thelathini na nne na senti hamsini (2,034,000.50/-) kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa ikiwa kama sehemu ya mchango wa Walimu Wakuu wa shule za Sekondari nchini kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya matope na mawe kutoka mlima Hanang’.
Waziri amepokea fedha hizo Disemba 19,2023 Ofisni kwake Jijini Dodoma, ambapo kwa Niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu amewashukuru walimu hao kwa mchango wao.
Jambo hili la maafa la maporomoko ya Matope na Mawe kutoka Mlima Hanang’ mafanikio yake yalipatikana na yameongozwa na utashi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Walimu ni Viongozi,na wamedhihirisha uongozi wao katika mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kutambua kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuunga mkono katika masuala mbalimbali.” Alisisitiza Waziri Mhagama.
Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa alisema Walimu hawa kwa ushirikiano wao Nchini “Waliona umuhimu wa kuchangishana na kusaidia waathirika wa maafa yaliyotokea Hanang’ na kunituma nikukabidhi wewe Waziri mwenye dhamana.”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Mhe. Jenista Mhagama akipokea mchango wa Walimu Wakuu wa shule za Sekondari nchini kwaajili ya waathirika wa maafa ya maporomoko ya matope na mawe kutoka mlima Hanang uliowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba yao.
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amepokea Fedha Taslimu kiasi cha Shilingi Milioni Mbili na elfu thelathini na nne na senti hamsini (2,034,000.50/-) kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa ikiwa kama sehemu ya mchango wa Walimu Wakuu wa shule za Sekondari nchini kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya matope na mawe kutoka mlima Hanang’.
Waziri amepokea fedha hizo Disemba 19,2023 Ofisni kwake Jijini Dodoma, ambapo kwa Niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu amewashukuru walimu hao kwa mchango wao.
Jambo hili la maafa la maporomoko ya Matope na Mawe kutoka Mlima Hanang’ mafanikio yake yalipatikana na yameongozwa na utashi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Walimu ni Viongozi,na wamedhihirisha uongozi wao katika mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kutambua kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuunga mkono katika masuala mbalimbali.” Alisisitiza Waziri Mhagama.
Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa alisema Walimu hawa kwa ushirikiano wao Nchini “Waliona umuhimu wa kuchangishana na kusaidia waathirika wa maafa yaliyotokea Hanang’ na kunituma nikukabidhi wewe Waziri mwenye dhamana.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...