NA MWANDISHI WETU,PEMBA.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis, amesema njia pekee ya wananchi wa Pemba kumshukru,kuthamini na kumuenzi Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi ni kumpa zawadi ya ushindi CCM wa Viti vya Urais,Ubunge,Uwakilishi na Udiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Hayo ameyasema wakati akizungumza na Wanachama wa CCM wa majimbo matano ya Wilaya ya Chakechake katika ukumbi wa ZSSF Tibirinzi, Mkoa wa Kusini Pemba.
Alisema kuwa maendeleo yaliyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Dk.Mwinyi, kielelezo pekee cha kuonyesha ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 kisiwani humo.
“Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi, amefanya mambo mengi ya maendeleo katika kisiwa cha Pemba hasa katika sekta ya utalii,michezo,afya,elimu,kilimo,uvuvi,utamaduni na kiuchumi hivyo wananchi wa kisiwa hiki hamna cha kumdai Rais wetu huyu na bado anaendelea kusimamia mambo mengi ya maendeleo.”, alifafanua Mbeto.
Mbeto, aliwakumbusha wanachama hao kuwa wajitokeze kwa wingi katika uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ili waingizwe katika mfumo rasmi wa wapiga kura wenyeb sifa kisheria.
Alisema kwamba ushiriki mzuri wa wanachama hao katika zoezi hilo ndio sehemu ya mikakati ya ushindi wa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Katika maelezo yake Katibu huyo Mbeto, aliwasisitiza wanachama hao kushuka ngazi mbali mbali za uongozi katika Chama na Jumuiya zake kuwahamasisha wanachama wa makundi mbalimbali washiriki kikamilifu katika zoezi hilo la uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura katika Wilaya hiyo. Kupitia mkutano huo Katibu huyo wa NEC Mbeto, aliwasisitiza wanachama hao kufuata maelekezo waliyopewa na viongozi mbalimbali katika kufuanikisha zoezi hilo ambalo ndio msingi wa kujitathimini kisiasa katika upangaji wa mikakati ya ushindi wa dola mwaka 2025.
Home
HABARI
WANANCHI PEMBA WATAKIWA KUMPA ZAWADI YA USHINDI RAIS DKT SHEIN UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...