Na Jane Edward, Arusha
Ni majira ya saa tano za asubuhi,kundi la warahibu pamoja na vikundi vya wasanii wanaotoka hapa Jijini Arusha wanakutana kwa pamoja na Taasisi ya kupambana na madawa ya kulevya na kupatiwa elimu juu madhara ya Matumizi ya madawa hayo.
Shauku ya Taasisi ya kupambana na madawa ya kulevya nchini ni kuona Vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa wanaacha matumizi ya madawa hayo ambayo yamekuwa yakififisha ndoto za vijana walio wengi.
Shaban Miraj ambaye ni afisa na msimamizi wa elimu ya Madawa ya kulevya taasisi ya kudhibiti Madawa ya kulevya Kanda ya kaskazini ambapo anasema wameamua kutoa elimu na mafunzo ya madhara ya madawa ya kulevya kwa makundi hayo kutokana na eneo la kanda ya kaskazini kuongoza kwa matumizi na kilimo cha madawa hayo.
"Sisi tunataka kuhakikisha Matumizi ya madawa ya kulevya kwa Warahibu hasa katika kanda ya kaskazini yanapungua kwa kiasi kikubwa na niwaombe wananchi wanapokuwa na ushahidi wa moja kwa moja watupigie kwa namba 119 ambayo ni bure''Alisema Miraj
Mkuu wa kitengo cha kutolea huduma saidizi kwa waraibu wa dawa za kulevya katika hospital ya mkoa wa Arusha Mount Meru Dr.Salum Saidi amesema ongezeko la dawa hizo kwa mkoa wa Arusha linachangiwa kwa kiasi kikubwa na nchi jirani kwa baadhi ya madawa kuruhusiwa jambo linalohitaji elimu ya ziada kwa wananchi.
"Wenzetu wa nchi jirani wao kwao matumizi ya madawa ya kulevya kama Mirungi ni jambo la kawaida sasa kutokana na ukaribu tulio nao uwezekano wa kuingiza hapa nchini ni mkubwa"Alisema
Denisi Mgie ni Afisa usitawi wa jamii mkoa wa Arusha ambapo anasema katika kutokomeza matumizi ya dawa za kulevya wamefanikiwa kuendesha operesheni mbalimbali za kukomesha biashara hiyo kwa kutumia wadau pamoja na mashirika binafsi.
Baadhi ya vijana Naomi Steven waliojitokeza kupatiwa elimu na mafunzo ya kutambua madhara ya matumizi ya madawa hayo wameishukuru mamlaka ya kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya kwa elimu hiyo kwakua ni waathirika wakubwa.
Amesema kama nguvu kubwa ikawekwa kwenye kuwatambua wauzaji wakubwa na kuwatia nguvuni ni dhahiri kuwa kwenye jamii waliopo hakutakuwa na watumiaji kwani wakiikosa wataishi vizuri na jamii inayo tegemewa.
Hata hivyo Katika kipindi cha Mwaka huu wamefanya opareshen katika maeneo ya Longido,Arumeru na Arusha mjini na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 14 na kufungua kesi 14 huku wakikamata bangi magunia 237,mbegu za bangi 310,pamoja na mirungi kilogram 1.534 pamoja na Heroin.
Mamlaka hiyo imetoa Rai kwa wadau pamoja na jamii kwa ujumla kushirikiana kwa pamoja kutokomeza matumizi ya Madawa hayo ili kusaidia kizazi Kijacho na kuwa na jamii yenye usawa.
Afisa Shaban Miraj ambaye ni msimamizi wa utoaji elimu Taasisi ya kupambana na madawa ya kulevya kanda ya kaskazini akitoa elimu kwa Warahibu wa madawa hayo.
Mkuu wa kitengo cha kutolea huduma saidizi kwa warahibu wa dawa za kulevya katika hospital ya mkoa wa Arusha Mount Meru Dr.Salum Saidi akizungumza na waandishi wa habari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...