Jumla ya Wakaguzi 15 kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) waliokuwa wanahudhuria kozi maalum(CAA Approval of Training organisations) ya wakaguzi wa vyuo vya usafiri wa anga iliyotolewa na shirika la usafiri wa anga duniani(ICAO) katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) wamemaliza kozi hiyo ya siku tano kwa ufaulu wa juu.

Akifunga kozi hiyo Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Aristid Kanje amewapongeza washiriki wa kozi hiyo na kuwahimiza wakitoka hapo wakaonyeshe umahiri wao sokoni kwani maarifa yanapimwa na utendaji kazi na sio ufaulu kwenye cheti.

Kanje aliongeza kuwa chuo cha CATC ni moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.

Kozi hiyo ya ICAO imeendeshwa na mtaalam aliothibitishwa na ICAO, Naomi Mwangi kutoka Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani upande wa mafunzo ya Usafiri wa Anga(ICAO TRAINAIR PLUS ).

Kozi hiyo iliyoanza Novemba 27, 2023 imemalizika Disemba 1,2023 imedhaminiwa na Mradi wa kuijengea Tanzania uwezo katika upande wa Usafiri wa Anga katika mifumo ya Usafiri wa Anga kutoka Jamhuri ya Watu wa China.
Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Aristid Kanje akizungumza na Wakaguzi 15 kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) waliokuwa wanahudhuria kozi maalum(CAA Approval of Training organisations) ya wakaguzi wa vyuo vya usafiri wa anga iliyotolewa na shirika la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO) katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
 Meneja Mradi wa kuijengea Tanzania uwezo katika upande wa Usafiri wa Anga katika mifumo ya Usafiri wa Anga wa Jamhuri ya Watu wa China Emanuael Mikongoti wa TCAA akizungumza kuhusu Mradi huo wakati wa kufunga Kozi maalum(CAA Approval of Training organisations) ya wakaguzi wa vyuo vya usafiri wa anga iliyotolewa na shirika la usafiri wa anga duniani(ICAO) katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa Wakaguzi 15 kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Naomi Mwangi kutoka Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani upande wa mafunzo ya Usafiri wa Anga (ICAO TRAINAIR PLUS) akizungumza  jambo wakati wa kufunga kozi maalum(CAA Approval of Training organisations) ya wakaguzi wa vyuo vya usafiri wa anga iliyotolewa na shirika la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO) katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Aristid Kanje (kulia) akimkabidhi zawadi Naomi Mwangi kutoka Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani upande wa mafunzo ya Usafiri wa Anga (ICAO TRAINAIR PLUS) wakati wa kufunga kozi maalum(CAA Approval of Training organisations) ya wakaguzi wa vyuo vya usafiri wa anga iliyotolewa na shirika la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO) katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Mkutano ukiendea
Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Aristid Kanje akiwakabidi vyeti Wakaguzi 15 kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) waliokuwa wanahudhuria kozi maalum(CAA Approval of Training organisations) ya wakaguzi wa vyuo vya usafiri wa anga iliyotolewa na shirika la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO) katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Aristid Kanje akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakaguzi 15 kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) waliokuwa wanahudhuria kozi maalum (CAA Approval of Training organisations) ya wakaguzi wa vyuo vya usafiri wa anga iliyotolewa na shirika la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO) katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...