Tuzo hiyo imekabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika Disemba mosi katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya TCAA Bw. Teophory Mbilinyi.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hii Bw. Mbilinyi amesema tuzo hiyo ina tija kubwa kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga na inawachochea katika utendaji wao.

"TCAA kama mdhibiti wa sekta ya usafiri wa anga tunao wajibu mkubwa katika kuhakikisha shughuli zetu zinachochea ukuaji wa uchumi wa taifa letu lakini hii inaanza kwa sisi kuwa mfano wa kuigwa na ndio maana ulipaji kodi ni kipaumbele chetu, tuzo hii inaendelea kutuchochea katika utendaji" amesema Bw. Mbilinyi.

Kwa mwaka wa pili mfululizo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetambua na kuitunuku tuzo TCAA kwa juhudi yake katika masuala ya kodi katika mkoa wa kikodi wa Ilala.
 
Naye Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata  amesema  wafanyabiashara wanapaswa kulelewa ili walipe kodi zaidi, wanapaswa kufundishwa umuhimu wa kulipa kodi, na kazi hii ni ya Wizara ya Fedha na TRA.

Alieleza kuwa, Serikali ya Awamu Sita itaendelea kufungua nchi ili kuvutia uwekezaji zaidi, kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji, pamoja na kupambana na kutokomeza rushwa ikiwemo kwenye sehemu zinazohusisha Wafanyabiashara.
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya TCAA Bw. Teophory Mbilinyi katikati akikabidhiwa cheti na Naibu kamishna Kodi za Ndani TRA, Edmond Kawamala  cha mlipaji kodi bora katika Mkoa wa Kikodi wa Ilala katika hafla fupi iliyofanyika Disemba mosi katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata akizungumzia hatua mbalimbaliz zilizotumika kuwapata washindi wa Tuzo kwa Walipakodi Bora kwa mwaka 2022/2023 wakati wa hafla fupi iliyofanyika Disemba mosi katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla fupi za Tuzo kwa Walipakodi Bora kwa mwaka 2022/2023 ziliyofanyika Disemba mosi katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja 
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya TCAA Bw. Teophory Mbilinyi azungumza na waandishi wa Habari kuhusu namna Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) walivyopata tuzo ya mlipaji kodi bora katika Mkoa wa Kikodi wa Ilala wakati wa hafla fupi iliyofanyika Disemba mosi katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...