Na Issa Mwadangala.


Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Thomas More Jimbo Kuu la Mbeya wametakiwa kuzishinda dhamiri zao mbaya ili kutotenda matendo uhalifu katika jamii.

Hayo yalisemwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya, Disemba 17, 2023 wakati aliposhiriki ibada hiyo ya misa takatifu na kutoa elimu kwa waumini walioshiriki ibada hiyo kuhusu madhara ya kutekeleza dhamiri mbaya akiwa anasisitiza mahubiri ya Padre Karolo Kavindi wa Parokia hiyo ambayo inapelekea kufanya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Kamanda Mallya alisema si jambo jema kwa muumini anayekuja kanisani kumcha Mungu lakini anatekeleza dhamiri mbaya ambayo inampelekea kufanya ukatili na vitendo vya uhalifu.

Kamanda Mallya aliongeza kuwa kumcha Mungu ni kuyatenda yale yote aliyoyaelekeza katika biblia na vitabu vitakatifu pia kuyaishi ili kutokomeza vitendo viovu katika jamii na hapo tutakuwa tumeishinda dhamiri mbaya ndani ya mioyo yetu.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...