Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Hamad Masauni akizungumza wakati wa akifungua Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi wa Dini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kamisaa wa Sensa Spika Mstaafu Anne Makinda akitoa maelezo kuhusiana matokea ya Sensa katika  Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi wa Dini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni aikiwa katika picha ya pamoja makamisaa wa Sensa pamoja na viongozi mara baada ya kufungua Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi wa Dini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

*Sensa yatumika kuratibu waathirika wa mafuriko

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
SERIKALI imesema kuwa katika matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi Mwaka 2022 kwa wadau wote watumie matokeo hayo katika mipango mbalimbali.

Hayo ameyasema Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni wakati wa akifungua Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi wa Dini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Masauni amesema mafunzo kwa viongozi wa dini yana umuhimu katika katika kupanga mipango ya maendeleo kwenye jamii.

Amesema kuwa kwa kutumia matokeo ya sensa katika kutoa maoni katika miradi mbalimbali kutokana na mahitaji yao.

Waziri Masauni amesema kuwa Sensa ya mwaka 2022 ilikuwa katika maeneo matatu ambayo ni Sensa ya Watu ,Majengo na Anuani za makazi ambapo maeneo hayo yote yanasaidia katika usalama wa nchi kwenye masuala ya uhalifu.

Masauni amesema Sensa iliyofanywa imesaidia katika mafuriko yaliyotokea Hanang kutokana na baadhi ya waathirika kuingiza vitu ambavyo havikuwemo na kubaini hayo imetokana na sensa ya mwaka 2022.

Amesema matokeo hayo ya sensa yataweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupanga shughuli mbalimbali za nchi katika kuleta Maendele mradi o yake ikiwemo kwenye masuala ya kiusalama.

"Serikali ilikuwa katika hatua ya utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kuimarisha usalama nchini hivyo basi matokeo haya ya sensa yalitokana na umuhimu wa kuhusisha maeneo matatu ikiwemo kuimarisha usalama nchini ili yawezw kufanikisha kwa urahisi,"amesema.

Aidha amesema dhamira serikali ni kuhakikisha inakamilisha mchakato wake wa miradi ya kiusalama katika miji minne mikubwa ambapo inaanza na Mkoa wa Dar es Salaam, Dodoma,Mwanza na Arusha ambapo katika mradi huo utahusisha matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kubaini uhalifu na wahalifu na kuweza kuwakabili kwa haraka.

Waziri Masauni amesema kwa namna hiyo nchi itaenda kufaidi matumizi ya takwimu ipasavyo kwa sababu itawezesha kufahamu kwa urahisi watu wale watakaofanya uhalifu kupatikana kiurahisi.

Amesema mafunzo hayo wanayoyatoa kwa Makundi mbalimbali yamekuwa na msaada mkubwa kwa watu kwani wamekuwa wakielimisha juu ya uwepo wa ramani ya maeneo yao na kuonyesha kila kitu ambapo inasaidia sasa wananchi kuwajibika kimaendeleo katika maeneo yao.

"Sensa ya mwaka 2022 imemalizika,Sasa nchi inajiandaa na nyingine ambapo hii inatusaidia kuonyesha kwa uhalisia maeneo gani ambayo hayajapata kipaumbele katika maendeleo kwani kuna baadhi ya vijiji viliomba kujengewa shule lakini unakuta watoto ni wachache ,unakuta Kiongozi mmoja alikuwa na sauti hivyo Kila kitu kinaenda kwake,"amesema na kuongeza.

"Hivyo sasa maeneo ambayo hayajapata kipaumbele ndo yatapewa kipaumbele na hapo tutauliza sensa inasemaje katika kupeleka Maendeleo katika eneo hilo,"amesema.

Aidha amesema kuwa viongozi wa dini wakitaka Taifa kutenda zambi ya kupasua taifa wanaweza kufanya hivyo wanatakiwa kusimama katika misingi ya imani na kukiuka kwake kwa kutafanya kurithisha viongozi wengine katika lililopasuka.

Kamisaa wa Sensa Spika Mstaafu Anne Makinda amesema kuwa viongozi wa dini walikuwa mstari mbele hakuna hata mtu mmoja aliyetaka watu wasijitokeza kuhesabiwa.

Kamisaa Makinda amesema Sensa iliyofanywa na kuja na matokeo ambayo yanakwenda kurahisha katika upangaji wa rasilimali kwenda katika maeneo husika.

Spika Mstaafu Makinda amesema kuwa matokeo ya sensa inakwenda kutoa majawabu maeneo yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.

Mratibu wa Sensa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Kapala amesema katika matokeo hayo NBS imekuwa ikielemisha makundi mbalimbali.

Amesema mafunzo hayo yanafanyika kwa mujibu wa mwongozo wa kitaifa wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

"Mwongozo huo umeeleza mafunzo haya yafanyike kuanzia ngazi ya taifa hadi ya chini kabisa za utawala kwa makundi mbalimbali, " amesema.

Kaimu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Waridi amesema mafunzo hayo yamekuja wakati mwafaka katika kwenda kupanga mipango kwenye kuhudumia wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...