Na Mwandishi Wetu, Ivory Coast

Mabingwa mara mbili wa Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON), Ivory Coast ambao ni wenyeji wa Michuano hiyo ya mwaka 2023 wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Guinea-Bissau katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa kwenye dimba la Alassane Ouattara mjini Abidjan.

Bao la kwanza la Côte d'Ivoire lilifungwa na Mchezaji wao, Seko Fofana kwenye dakika 4’ baada ya kuunganisha mpira safi uliomshinda Golikipa wa Guinea-Bissau, Ouparine Djoco. Bao la pili lilifungwa na Jean Philippe Krasso kwenye dakika ya 58’ ya mchezo huo.

Mchezo huo wa kwanza wa ufunguzi wa Kundi A, ulioshuhudiwa na Rais wa Shirikisho la Soka duniani (FIFA), Gianni Infantino, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, Dkt. Patrice Motsepe. Pia umeshuhudiwa na mashabiki lukuki wa soka barani Afrika na nje ya Afrika.

Wenyeji, Ivory Coast wameanza vyema mashindano hayo wakiwa kinara kwenye Kundi A wakiwa na alama tatu, wapo pamoja na timu za Nigeria, Equatorial-Guinea na Guinea-Bissau.

Burudani mbalimbali za Wasanii kutoka kona mbalimbali, kina Franco-Ivorian, Magic System, Yemi Alade (Nigeria) na Rapa kutoka nchini Misri, Mohamed Ramadan walishuhudiwa wakiingia kwenye historia ya kusherehesha kuanza kwa mashindano hayo ya 34 tangu kuanzishwa kwake.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...